Home » » Mbunge Nyambari Nyangwine awataka vijana kutumia fursa walizonazo kujikwamua na lindi la umaskini.

Mbunge Nyambari Nyangwine awataka vijana kutumia fursa walizonazo kujikwamua na lindi la umaskini.

Written By JAK on Thursday, January 2, 2014 | 10:30 PM


Mbunge wa Jimbo la Tarime (CCM),Mh.Nyambari Nyangwine ambaye pia alikuwa ndiye mgeni rasmi akizungumza machache kwenye kilele cha tamasha la Krismasi na Mwaka mpya lililofanyika jana jioni kwenye uwanja Jamhuri mkoani Dodoma,Mh Nyangwine alitumia fursa yake ya kuwataka Watanzania kuwa watulivu,wenye kuendelea kujenga mshikamano ili kuendelea kuidumisha amani ya nchi walionayo,pia amewataka vijana popote pale walipo kuacha kulalamika kuhusu suala la ajira na kutumia fursa walizonazo,kwani serikali haiwezi kuwapa ajira wote nchini,Badala yake wajitume na kujiajiri wenyewe katika suala zima la kujikwamua na lindi la umaskini.Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions Ltd,Bwana.Alex Msama. 
 Vijana wakali wa Vocal,The Voice wakiimba jukwaani jana jioni kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma wakati wa kilele cha tamasha la krismasi na Mwaka Mpya.
Waimbaji mahiri wa nyimbo za Injili pichani kulia ni  Edson Mwasabwite,Tumaini Njole na Faraja Ntaboba kutoka nchni Congo-DRC wakilishambulia jukwaa kwa pamoja kwenye kilele cha tamasha la Krismasi na Mwaka mpya mkoani Dodoma.
 Sehemu ya umati wa watu waliofika kwenye tamasha jana jioni  ndani ya uwanja wa Jamhuri.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger