Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akipokewa na walimu wa Philter Federal School
ya Fuoni Meli Tano kwenye hafla ya wazazi wa skuli hiyo pamoja na maadhimisho
ya kutimia miaka Mitano ya Skuli hiyo.
Baadhi ya Wazazi waliohudhuria hafla wazazi na maadhimisho ya
miaka Mitano ya Federal School ya Fuoni Meli tano zilizofanyika Hoteli ya
bwawani Mjini Zanzibar.
Wanafunzi wa Maandalizi wa
Federal School ya Fuoni wakionyesha umahiri wao katika kudumisha utamaduni wa
Zanzibar ukianmbata na vazi maarufu la Kanga ya Kisutu.Picha na
Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
========= ======== =======
Mke wa
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi ameiasa Jamii kwamba
uigaji wa hulka na Tabia za kigeni zinazoonekana kulikumba zaidi kundi kubwa la
Vijana unazalisha malezi mabovu yanayokwenda kinyume na Utamaduni wa Taifa
hili.
Kauli hiyo
aliitowa kwenye halfa ya mahafali ya wazazi pamoja na maadhimisho ya kutimia
miaka mitano ya Philter Federal School
iliyopo Fuoni Meli Tano nje kidogo ya Mji wa Zanzibar zilizofanyika
katika ukumbi wa Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar.
Mama Asha
alisema wakati dunia inaendelea kupitiwa na mabadiliko makubwa ya mitandao ya
Teknolojia wazazi wanapaswa kuwa makini
kipindi hichi cha mpito katika kufuatilia nyendo za watoto wao.
Alisema
licha ya muda mwingi wa watoto hao unakuwa ndani ya himaya ya walimu lakini
bado Wazazi wanawajibu mkubwa wakuhakikisha wanashirikiana na walimu hao katika kuwafinyanga watoto wao kuelekea
katika njia sahihi. Katika
kuimarisha kiwango cha elimu maskulini hasa kwa zile skuli za binafsi zinazojitegemea
zenyewe Mama Asha alisema wazazi wahakikishe wanalipa ada za watoto wao kwa wakati ili kutoa nafasi
kwa walimu kuendelea kusomesha kwa utulivu.
Aliupongeza
Uongozi wa Philter Federal School kwa juhudi unaochukuwa wawafinyanga watoto
wao na kuwa mahiri kimasomo na hata ushiriki wao wa michezo mbali mbali.
Mke huyo wa
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuahidi Uongozi wa Skuli hiyo kwamba
atakuwa tayari kusaidia nguvu za skuli hiyo katika kuona lile lengo
walilojipangia la kutoa elimu bora na safi linafanikiwa vyema.
Akisoma
Risala ya Skuli hiyo Mwanafunzi Hassan Hassan Lukoma alisema yapo mafanikio
makubwa yaliyopatikana ndani ya skuli hiyo katika kipindi cha miaka mitano
tokea ilipoanzishwa mwaka 2009.
Mwanafunzi
Hassan alisema Philter Federal School imekuwa ikiendelea kutoa wanafunzi mbali
mbali wa michepuo kuingia kiwango cha sekondari katika masomo ya sanaa, Sayansi
pamoja na biashara.
Alisema
katika kuimarisha ufaulu wa wanafunzi wa Skuli hiyo juhudi zimechukuwa na
uongozi wa skuli hiyo katika kujiandaa na ufundishaji wa Lugha za kigeni
zitakazotoa furtsa na wigo wa kuimarika kwa kiuchumi kutokana na kukomaa kwa
kiwango cha elimu Kimataifa.
Hata hivyo
mwanafunzi Hassan Hassan alizitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili skuli
hiyo kuwa ni pamoja na upungufu wa vifaa vya sayansi, uhaba wa vikalio pamoja
maslahi duni ya walimu kutokana na wazazi kuchelewa kulipa ada za watoto wao.
Mapema
Mkurugenzi Utumishi Wizara ya Elimu an maafunzo ya Amali Zanzibar Nd. Vuai
Khamis Juma alisema katika kusaidiana na Skuli Binafsi Wizara ya Elimu imeandaa
utaratibu maalum wa kugawa vitabu ilivyonavyo kwa kuzipatia skuli binafsi.
Nd. Vuai
alitoa wito kwa walimu wa skuli hiyo kusomesha kwa bidii na uadilifu na
kuwaomba wanafunzi wao kuepuka tabia ya kughushi mitihali yao jambo ambalo
litachangia kuviza kiwango cha elimu
pamoja na upatikanaji wa wataalamu waliobobea.
Katika hafla
hiyo iliyoshuhudiwa na wazazi kadhaa wa wanafunzi Mama Asha alikabidhi vyeti kwa wanafunzi wa Skuli ya Maandalizi na
wale wa Darasa la kumi na mbili { Form IV } waliomaliza masomo yao. Pia hafla
hiyo ilijumuisha michezo mbali mbali iliyochezwa na wanafunzi hao wa maandilizi
na Sekondari wakionyesha umahiri wao uliotoa burdani safi katika viunga vya
Hoteli ya Bwawani.
Othman
Khamis Ame
Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
6/1/2014.
Post a Comment