Mwakilishi
wa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraim Kwesigabo akitoa
maelezo ya utangulizi katika ufunguzi wa mafunzo ya wiki mbili ya Wakufunzi wa
Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 yaliyofanyika leo katika
ukumbi wa Edema uliopo Morogoro mjini.
Naibu Waziri wa Kazi na
Ajira Mhe. Dkt. Milton Mahanga (MB) akihutubia wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya
wiki mbili ya Wakufunzi wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka
2014 yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Edema uliopo Morogoro mjini.
Naibu Waziri wa Kazi na
Ajira Mhe. Dkt. Milton Mahanga (MB) akihutubia wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya
wiki mbili ya Wakufunzi wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka
2014 yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Edema uliopo Morogoro mjini.
Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Dkt. Milton Mahanga (katikati) akiwa katika picha ya pamoja baada ya kufungua
rasmi Mafunzo ya wiki mbili ya Wakufunzi wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa
Kufanya Kazi wa mwaka 2014 yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Edema uliopo
Morogoro mjini. (Picha zote na Veronica
Kazimoto – Morogoro).
=========
======= ======
OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
YAWANOA WAKUFUNZI WA UTAFITI WA WATU WENYE UWEZO WA KUFANYA KAZI
(Na Veronica kazimoto –
Morogoro)
06 Januari, 2014.
Ukosefu wa Ajira umekuwa ni
changamoto kubwa kwa sasa duniani kote ambapo ripoti ya mwaka 2013 ya Shirika
la Kazi Duniani (ILO) kuhusu hali ya ajira duniani, inaonesha kuwa
takribani watu milioni 197 sawa na asilimia 5.9 ya nguvu kazi duniani
hawana kazi.
Hayo yamesemwa na Naibu
Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Dkt. Milton Mahanga wakati akifungua
Mafunzo ya Wakufunzi wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka
2014 yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Edema uliopo Morogoro mjini.
Dkt. Mahanga amesema kati
ya watu 197 ambao hawana kazi vijana ni milioni 73.8 sawa asilimia 12.6 ambayo
ni nguvukazi inayopaswa kutumika ipasavyo kwa kuwa kuna mahusiano makubwa kati
ya ukuaji wa tija na matumizi ya nguvukazi. Ameongeza kuwa, kutokana na
changamoto hiyo ya ajira, ni muhimu kufanya Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa
Kufanya kazi ili kuisaidia Serikali kufuatilia mwenendo wa mabadiliko
yanayotokea katika soko la ajira.
Mahanga amefafanua kuwa
utafiti huu utasaidia pia kuboresha sera na program mbalimbali za kukuza ajira,
kupanga na kufuatilia utekelezaji wa mipango ya maendeleo kama vile Malengo ya
Milenia, Dira ya Maendeleo ya mwaka 2015 na Malengo ya MKUKUTA na MKUZA. Kwa upande wa Mwakilishi wa
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Ephraim Kwesigabo amesema lengo
kuu la Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi ni kukusanya takwimu
zinazohusu hali ya soko la ajira nchini.
Kwesigabo amesisitiza kuwa
utafiti huo utawezesha kupata viashiria vinavyohusu ajira na ukosefu wa
ajira kwa makundi mbalimbali yaliyopo katika jamii na hivyo kuisaidia Serikali
kuboresha sera ya kukuza ajira nchini. Mafunzo hayo ya wiki mbili yameandaliwa
na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ambapo jumla ya Wakufunzi 60 kutoka mikoa
mbalimbali nchini wanaendelea kupewa mafunzo juu ya Utafiti huo wa Watu
Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi utakaoanza rasmi mwezi Februari hadi Disemba mwaka
2014.
Post a Comment