Home » » DR BILAL AFANYA ZIARA YA KUKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO DAR NA MAENDELEO YA UJENZI WA DARAJA LA MPIJI

DR BILAL AFANYA ZIARA YA KUKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO DAR NA MAENDELEO YA UJENZI WA DARAJA LA MPIJI

Written By JAK on Monday, April 14, 2014 | 12:23 AM



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Eng. Mussa Iombe, sehemu ya Daraja la Mpiji linalounganisha Bagamoyo na Dar es Salaam, lililokatika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini, wakati Makamu alipofanya ziara hiyo ya kujionea maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo leo Aprili 13, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wanaosimamia shughuli ya daraja hilo, baada ya kuwasili eneo hilo leo.

Sehemu ya daraja hilo, linavyoonekana baada ya kuongezeka upana kwa kulika kutoka mita 25 na sasa kufikia mita 75, ambapo tayari Malori yameanza kumwaga vifusi vya mawe ili kuziba eneo hilo na kuweza kuunganisha njia hiyo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi kuelekea eneo la tukio kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mpiji lililokatika kutokana na Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini.
  
 Malori yakimwaga vifusi vya Mawe kwenye daraja hilo.
 
Nguzo za umeme zikiwa zimeinama baada ya kuzidiwa nguvu na maji hayo yaliyobomoa daraja.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa maelekezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Eng. Mussa Ibrahim Iombe, wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mpiji lililokatika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini.Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuhitimisha ziara yake hiyo, katika eneo la Daraja la Mpiji, linalounganisha Bagamoyo na Dar es Salaam, leo Aprili 13, 2014.
 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiondoka eneo la tukio Daraja la Mpiji baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja hilo lililokatika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini. Picha na OMR
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger