Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa Viongozi wote wa Chadema waliokwenda Kituo cha Wilaya
cha Polisi Mjini Arusha Mwenyekiti wa Mkoa Samsoni Mwigamba na Mwenyekiti wa Chadema
Wilaya
ya Arusha Ndg Golugwa ,wameshaondoka eneo la Polisi usiku huu , wakirudi kwenye eneo linalofanyikia Mkutano Corridor Spring Arusha.
Kikao hicho kinaongozwa na Mwenyekiti wa Chadema na Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni
Mh. Mbowe ,kikihudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Arusha Ndg Lema G., Mbunge wa Karatu
na viongozi wengine wa Chama hicho.
KIKAO KINAENDELEA.
Mwanahabari wetu anawasiliana na uongozi wa Chama hicho ili
kuwaletea habari
kamili mara atakapowapata.
Post a Comment