Home » » WALIOPORA MAITI WAHUKUMIWA JELA MIAKA 120

WALIOPORA MAITI WAHUKUMIWA JELA MIAKA 120

Written By JAK on Friday, October 25, 2013 | 1:21 AM

Gari aina ya Land cruiser mali ya chuo cha SUA cha mjini Morogoro kama linavyoonekana baada ya kupigwa mawe na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi  nje kidogo ya mji wa Singida.
 Kesi inayowakabili washitakiwa watano walioteka gari la chuo cha SUA mjini Morogoro na kunyang’anya zaidi ya shilingi 19.8 milioni, hukumu yake inatarajiwa kutolewa kesho na mahakama ya wilaya ya Singida. Utekaji huo ulifanyika Desemba sita mwaka jana saa saba na nusu usiku kwenye barabara kuu ya Dodoma – Singida eneo la Kisaki manispaa ya Singida.
Mhudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa mjini Singida ambaye jina lake halikuweza kutambuliwa mara moja,akiliweka sawa baada ya kufanyiwa ukarabati baada ya kubomolewa na majambazi na kulisachi.

KESI inayowakabili washitakiwa watano ya utekaji wa gari la chuo cha SUA Morogoro mjini na kisha kunyang’anya zaidi ya shilingi 19.8 milioni hukumu yake inatarajiwa kutolewa kesho na Mahakama ya Wilaya ya Singida.

Hukumu hiyo inayovutia hisia za wakazi wengi wa Manispaa ya Singida na vitongoji vyake inatarajiwa kusomwa na hakimu wa Wilaya ya Singida Flora Ndale.

Washitakliwa hao inadaiwa baada ya kufanikiwa azma yao ya unyang’anyi wa kutumia silaha za jadi waliweza kufungua jeneza lililokuwa linasafirisha mwili wa mwanafunzi wa SUA Munchari Lyoba na kulisachi kwa imani kwamba kuliwekwa mali.

Washitakiwa hao vijana ni Idd Omari (37),Khalid Hamisi (20), Abubakari Jumanne (25) wote wakazi wa kijiji cha Kisaki Manispaa ya Singida Wengine ni Hamisi Issa (32) mkazi wa kijiji cha Unyamikumbi na Amosi Ally (22) mkazi wa kijiji cha Mtakuja.

Washitakiwa hao wanatuhumiwa kuteka gari linalomilikiwa na SUA lenye namba za usajili SU 37012 ambalo siku ya tukio lilikuwa linaendeshwa na Kalistus Malipula.

Washitakiwa hao waliteka gari hilo desemba sita mwaka jana saa saba na nusu eneo la kijiji cha Kisaki Gari hilo lilikuwa linasafirisha mwili wa mwanafunzi Lyoba kwenda kuzikwa mkoani Mara.

HABARI YA HUKUMU

Mahakama ya Wilaya Singida imewahukumu watu wanne kutumikia vifungo vya miaka 120 jela kwa kuteka gari lililokuwa likisafirisha maiti kutoka mkoani Morogoro kwenda Musoma mkoani Mara na kupora waombolezaji kompyuta na fedha. Waliohukumiwa vifungo hivyo kila mmoja miaka 30 jela ni Hamis Ali (23), Hamisi Issa (33); Khaldi Hamis (21) na Abubakari Jumanne (26), wakazi wa Kisaki Manispaa ya Singida. Mshtakiwa wa kwanza Iddi Omari (38), aliachiwa huru baada ya mahakama hiyo kukosa ushahidi wa kumtia hatiani. Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Flora Ndale, alisema ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka bila kuacha shaka umethibitisha washtakiwa hao walitenda kosa hilo. 

Awali, Mwendesha Mashtaka,Sajini, Godwel Lawrence, alidai kuwa Desemba 6, mwaka 2012, saa 7:30 mchana, eneo la Kisaki, washtakiwa hao waliteka gari lenye namba za usajili SU 37012 aina ya Toyota Land Cruiser mali ya serikali lililokuwa likiendeshwa na Kalistus Malipula, wakati limebeba mwili wa Munchari Lyoba aliyefariki dunia akiwa mwanafunzi mwaka wa tatu Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (Sua) kwa ajili ya kuusafirisha kutoka Morogoro kwenda Musoma mkoani Mara kwa maziko

Alidai baada ya washtakiwa hao kuteka gari hilo waliwapora waombolezaji vitu mbalimbali zikiwamo kompyuta mpakato, simu za mkononi na fedha taslim zaidi ya Sh. milioni 8.7.

Alidai pia walivunja jeneza na kuufanyia upekuzi mwili wa marehemu huyo kwa kuchana sanda wakidhani kulikuwa na fedha zilizofichwa.

Kwa upande wao, washtakiwa hao waliiomba mahakama iwapunguzie adhabu kutokana na kutofanya kosa hilo, umri wao kuwa mdogo na wanategemewa na familia zao. Ombi hilo lilipingwa na mwendesha mashtaka na kuiomba mahakama kutoa adhabu kali ili liwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.

Hakimu Ndale alisema kosa lililofanywa na washtakiwa hao ni la kinyama na lisingeweza kuvumilika katika jamii, hivyo ili liwe fundisho kwa wote wanaofikiria kufanya vitendo vya kinyama kama hicho, anawahukumu kila mmoja kutumikia kifungo cha miaka 30 jela.

CHANZO: NIPASHEInadaiwa washitakiwa hao walitumia silaha za jadi ikiwemo fimbo na mawe kufanikisha azma yao hiyo Waliweka mawe makubwa barabarani kwa lengo la kuzuia magari kupita.

Soma Hapa Taarifa ya awali

Watu wasiofahamika idadi yao na ambao wanadhaniwa kuwa ni majambazi, wamevamia gari lililokuwa linasafirisha maiti kutoka Morogoro mjini hadi mkoa wa Mara na kupora zaidi ya shilingi milioni 19.8.

Baada ya kumaliza zoezi la uporaji huo, majambazi hayo yalishusha jeneza na kisha... kulifumua na kuanza kulisachi.

Jeneza hilo lilikuwa limebeba mwili wa mwanafunzi Munchari Lyoba, mwanafunzi wa mwaka wa tatu aliyekuwa anasomea elimu ya biashara kwenye chuo cha SUA.

Amesema gari hilo lilibeba viongozi wa wanafunzi sita na viongozi wengine wanne akiwemo dereva.

Akizungumza na waandishi wa habari leo nje ya chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya mkoa wa Singida, mkuu wa msafara huo Makarang Nouna, amesema tukio hilo limetokea Disemba 6 mwaka huu saa 7.30 usiku, na lilihusisha gari Land Curise lenye namba za usajili SU 37012 na lilikuwa likiendeshwa na Kalistus Malipula.

Amesema tukio hilo la kinyamana la kusikitisha, limetokea katika barabara kuu ya Dodoma – Mwanza nje kidogo ya mji wa Singida kwenye kona maarufu kwa jina la Mohammed Trans.

Amesema walipofika eneo la tukio, walikuta mawe makubwa yamepangwa kukatisha barabara, kitendo kilichosababisha washindwe kupita, na hivyo kutoa mwanya kuvamiwa na kundi kubwa la vijana ambao walibeba bunduki mbili aina ya gobore, marungu, mashoka na mawe.

Makaranga amesema walichofanya kwanza ni kupiga kioo cha gari letu kwa mbele, na baadaye kumparaza kwa panga usoni dereva wetu Kalistus Malipula.

Baada ya hapo walivunja vunja vyoo vyote na kutuamuru kutoa kila kitu ambacho tulikuwa nacho.

Akifafanua zaidi, amesema kwa upande wake yeye ameporwa shilingi milioni mbili ambazo zilikuwa kwa ajili ya kugharamia msafara huo, jumla ya shilingi milioni 8.8 ambazo zilichangwa na wanafunzi kama rambi rambi kwa mwenzao, na shilingi milioni tisa ambazo wasindikizaji walikuwa nazo zikiwa ni posho.

“Pia tumeporwa simu zetu zote za mikononi, viatu, laptop na mabegi yote ya nguo zetu”amesema.

Makaranga ambaye amesema anafanya kazi za kiutawala katika chuo cha SUA, amewataja walioumizwa zaidi ni pamoja nay eye, dereva Malipula na kiongozi wa wanafunzsi Idd Idd na kutibiwa katika hospitali ya mkoa na kuruhusiwa.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Singida Mwalimu Queen Mlozi, ambaye aliwasiliana na uongozi wa SUA Morogoro kwa ajili ya shughuli ya kutuma gari jingine na ukarabati wa jeneza, amesema kuwa kwa ushirikiano wa jeshi la polisi na kamati ya ulinzi na usalama, watahakikisha watu waliofanya unyama huo, wanakamatwa mapema iwezekanavyo ili waweze kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger