AFANYA MIKUTANO YA HADHARA MJINI SONGEA
Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa barabara ya lami ambayo inamaliziwa kujengwa yenye urefu wa mita 600 iliyopo katika Kata ya Mjini, Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma. Barabara hiyo imegharimu zaidi ya Sh75 milioni. Dk Nchimbi yupo mjini Songea kwa ziara ya siku tano akikagua pamoja na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo jimboni mwake.
Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (aliyevaa miwani) akiwa na Diwani wa Kata ya Mjini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Ruvuma, Joseph Fuime (kulia kwa Dk Nchimbi) wakipita kwa furaha barabara aliyoizindua Dk Nchimbi mjini Songea mkoani mjini Songea leo. Barabara hiyo yenye kiwango cha lami ina urefu wa mita 600 ambayo imegharimu zaidi ya Sh75 milioni, pia mbunge huyo ameweka jiwe la msingi katika ofisi ya Kata ya Mateka. Dk Nchimbi pia anatarajiwa kuzindua ujenzi wa mabweni ya sekondari pamoja na nyumba za walimu.
Sehemu ya mamia ya wananchi wa Kata ya Mjini, Manispaa ya Songea wakiwa tayari kwa kumsikiliza Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi. Dk Nchimbi baada ya kuzindua barabara yenye kiwango cha lami yenye urefu wa mita 600 ambayo imegharimu zaidi ya Sh75 milioni, pia mbunge huyo ameweka jiwe la msingi katika ofisi ya Kata ya Mateka. Dk Nchimbi katika ziara yake ya siku tano jimboni humo, pia anatarajiwa kuzindua ujenzi wa mabweni ya sekondari pamoja na nyumba za walimu.
Dereva wa bodaboda (pikpiki) akinyanyuliwa juu kwa furaha na wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi baada ya Mbunge wao kuyajibu maswali yake. Mamia ya wananchi waliohudhuria mkutano huo uliofanyika katika Kata ya Mjini, Manispaa ya Songea walipewa nafasi ya kumuuliza mbunge wao maswali mbalimbali.Dk Nchimbi baada ya kuzindua barabara yenye kiwango cha lami yenye urefu wa mita 600 ambayo imegharimu zaidi ya Sh75 milioni, pia mbunge huyo aliweka jiwe la msingi katika ofisi ya Kata ya Mateka. Dk Nchimbi katika ziara yake ya siku tano jimboni humo, pia anatarajiwa kuzindua ujenzi wa mabweni ya sekondari pamoja na nyumba za walimu.
Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akilifungua jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Mateka iliyopo mjini Songea mkoani Ruvuma. Dk Nchimbi pia alizindua barabara yenye kiwango cha lami yenye urefu wa mita 600 ambayo imegharimu zaidi ya Sh75 milioni iliyopo katika Kata ya Mjini, Manispaa ya Songea. Dk Nchimbi yupo mjini Songea katika ziara ya siku tano ya kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni humo.
Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza na mamia ya wananchi wa Kata ya Mateka, Mjini Songea baada ya kuizindua barabara yenye kiwango cha lami yenye urefu wa mita 600 ambayo imegharimu zaidi ya Sh75 milioni iliyopo katika Kata ya Mjini na baadaye kuweka jiwe la msingi katika ofisi ya Kata ya Mateka. Dk Nchimbi katika ziara yake ya siku tano jimboni humo, pia anatarajiwa kuzindua ujenzi wa mabweni ya sekondari pamoja na nyumba za walimu.
Post a Comment