Home » » WAZIRI MKUU,MIZENGO PINDA AENDELEA NA ZIARA YA KIKAZI NCHINI CHINA

WAZIRI MKUU,MIZENGO PINDA AENDELEA NA ZIARA YA KIKAZI NCHINI CHINA

Written By JAK on Saturday, October 26, 2013 | 2:13 AM


AWAONYA WATANZANIA “WASIJILIPUE”

 WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameawaonya baadhi ya Watanzania wanaokuja katika jiji la 
Guangzhou nchini China kwa ajili ya kununua bidhaa mbalimbali waache kuuza hati zao za kusafiria
 kwa raia wa nchi nyingine kama njia ya kujiongeza kipato. 

 Ametoa onyo hilo jana usiku (Alhamisi, Oktoba 24, 2013) wakati akizungumza Watanzania 
wanaofanya biashara na wale wanaoishi katika jiji la Guangzhou, jimbo la Guangdong ambalo
 ni jiji kubwa la biashara lililoko kusini mwa China. 

 Alisema kuwa wengi wa wafanyabiashara hao wanapouza pasipoti zao wanasingizia kuwa 
zimepotea ndio maana kuna malalamiko mengi kutoka kwa Watanzania wanaofika katika 
jimbo hilo kudai wanaibiwa hati zao za kusafiria wakati sio kweli. 

 Wakati wa mazungumzo hayo, mmoja wa Watanzania hao aliyejitambulisha kwa jina la
 Ambrose Lugai alisema changamoto nyingi zinazowakabili Watanzania waishio katika
 jimbo hilo na moja ya tatizo hilo ni kuibiwa kwa hati za kusafiria za Watanzania.

Bw. Lugai alisema tatizo la wafanyabiashara wengi kupoteza pasipoti limekuwa sugu 
na kila siku linaongezeka na cha ajabu linawatokea wafanyabiashara wa kutoka Tanzania tu. 

 “Hatuwezi kusema ni u-carelessnes, lakini jamii ya hapa ni kutoka mataifa mbalimbali, 
inakuwaje pasipoti za Tanzania tu ndio zinakuwa hot cake, naomba utusaidie namna ya 
kulinda hati hizi,” alisema Bw. Lugai. 

 Alimwomba Waziri Mkuu awasaidie kuzungumza na Serikali ya jimbo hilo ili Watanzania wawe
 wanaacha pasipoti hotelini wakati wanapoenda mitaani, badala yake wapewe karatasi 
nyingine ya kuwatambulisha huko mitaani.

Katika kujibu hoja hiyo ya Bw. Lugai, Waziri Mkuu alisema kwamba suala hilo linamshangaza 
kwamba inakuwaje hati za wafanyabiashara wa Tanzania tu ndio zinaiibiwa wakati 
wafanyabiashara wanaofika kwenye jimbo hilo ni wengi kutoka mataifa mbalimbali. 

“Kupoteza pasipoti ni jambo la nadra sana, sio la kawaida. Nilitegemea hili linaweza kumtokea
 mtu mmoja mmoja, lakini nashangazwa kwamba hapa Goangzhou ni tatizo kubwa.”

“Lakini taarifa nilizo nazo nyie wenyewe wafanyabiashara mnauza hati zenu kwa Wanaigeria ili 
mpate fedha za kufanyia biashara. Ndio maana nawasihi achani haya mambo, mnajifedhehesha 
wenyewe na mnaifedhehesha nchi,” alisema Waziri Mkuu. 

 Alisema kwa kuwa tatizo hilo ni kubwa na akamtaka balozi wa Tanzania nchini China, 
Luteni Jenerali mstaafu Abdulrahman Shimbo afuatilie kwa karibu kujua idadi ya watu w
alioibiwa hati zao za kusafiria ili Serikali iweze kulishughulikia. 

“Lakini nawaonya acheni tabia mbaya ya kuuza pasipoti zenu kwa tamaa ya kupata 
vijipesa vidogo vidogo hivyo, hii ni kuivunjia nchi heshima,” alisema. 

 Lakini pia alitaka jumuiya ya Watanzania waishio China kuimarishwa zaidi ili wawe na 
uwezo wa kushughulikia kero zao mbalimbali zinazowakabili wakiwa katika ugenini. 

Alisema ni kuimarika kwa jumuiya hiyo tu kutawasaidia wanafunzi na wafanyabiashara
 kufikisha malalamiko yao haraka serikalini. 

 IMETOLEWA NA: 
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
IJUMAA, OKTOBA 25, 2013
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh_akJbJdA0mJ2HZaOSsRIzJoez8Aro5fHwuMwJMUGD36hjMTvwrUPCdZKI_AotT7EbVnuPsjqLXIWfEBHD7GolnmZnwLfdQnEeAP58-cajIUVYjHI5nX3pi3SxQKS8jy_jaaC2pIDHqGtn/s1600/IMG_0725.JPG
Waziri Mkuu, mizengo Pinda akiongozana na Mwenyekiti wa shirika la Ndege la China la HAINAN AIRLINES, Bw. Chen Feng (kushoto na Balozi wa China nchini Dr. Lu baada ya mazungumzo yao kwenye hoteli ya Dong Fang mjini Guanzhou akiwa katika ziara ya kikazi nchinio China Oktoba 24, 2013.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEil6erLs9H5xaqKZvTG1t5v-VO0vxyfbglaBISTApT086sALTsLksFBr4WrIUSBRU8tMs2LEBCrT96n8mords3M1djZeAAya-Yo0Kc_rNbZzd3W_Y78u3-ahorMtAu6p1CI_8ZWGljpUyyR/s1600/IMG_0733.JPG
Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harison Mwakyembe akibadilishana kadi za mawasiliano na Rais na Mtendaji Mkuu wa  Shirika la Ndege la China Southern Air, Bw. Tan Wengeng wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na ujumbe wake walipokutana na Rais uyo kwenye Hoteli ya Dong Fang mjni Guanzhou China Oktoba 24, 2013.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh6PK8Zf0XJosGPWuu9jnR4Rf8Q3BTA_gcy7zDNPQw_h8LUsnhKVzl4Xd0MV5gQauiEFIuuMvsy59ULVKKxqXdnU4BZtH1BURmzw_iGKXQsSepjUduX6ffNJpcs5EYLX29Wdq6V01xh5iei/s1600/IMG_0757.JPG
Waziri Mkuu, MIzengo Pinda akisalimiana na Gavana wa jimbo la Guangdong nchini China, Bw. Zhu Xiaodan kabla ya mazungungumzo yao kwenye hoteli ya Dong Fang mjini Guanzhou akiwa katika ziara ya kikazi  nchini China Oktoba 24, 2013.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiXyEmGrw2n-7DRtEMW1JC1gcCq-CSfSQbntMvDtWpqETVj8oSXATNAvujuXQqHntqJMvFme_W8RGmI9yEgCYli0LtrFLQp9g8UZQU04_Imap74q9bwZA-4gK5nGZsLeGMwvUfTxPhSZn0M/s1600/IMG_0840.JPG
Watanzania wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipozungumza nao mjini Guanzhou China akiwa  katika ziara ya kikazi Oktoba 24,2013.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh9VZb5FCwowoHqHUu20yLZNImcp6bg1-MZgZ1tO2762pNHi3cTJydO01xNqQ28V00UKBmg5RrvRPmEs9yYQHlJpbqfFDYQcjKCefIBL_YlO4JnEOgDnJuSUF6606MFZ7BdtPwnjDaLWf3-/s1600/IMG_0828.JPG
Rais wa Umoja wa Watanznia waishio Guanzhou China, John Rwehumbiza akitembea haraka kuwahi mkutano  kati ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na watanzania waisio Guanzhou Oktoba 24, 2013.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiuajM_mrDLrP1hhU9zkOV58EdScPd_Q9iEjVaEcQds-OUPpuXzwzdwgGquun0cedKEIehdKWBW7DZWm0bN1HNIDUP51UOxFGNf7iM-momCPTYiyufseSWDO8Y8vwbvzcrGrXiXW9LEWdZt/s1600/IMG_0878.JPG
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Watanzania waishio Guanzhou China baada ya kuzungumza nao akiwa katika ziara ya kikazi nchini China Oktoba 24, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger