Home » » KINANA AMALIZA ZIARA YAKE WILAYANI TUNDURU KWA KISHINDO,KESHO KUANZA WILAYA YA NAMTUMBO MKOANI RUVUMA.

KINANA AMALIZA ZIARA YAKE WILAYANI TUNDURU KWA KISHINDO,KESHO KUANZA WILAYA YA NAMTUMBO MKOANI RUVUMA.

Written By JAK on Monday, November 18, 2013 | 5:21 AM


Pichani kulia Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana  akihitimisha ziara yake mapema leo jioni kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Baraza la Iddi,Wilayani Tunduru mkoani Rukwa na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu.Kinana na Ujumbe wake kesho ataelekea Wilayani Namtumbo kuendelea kukagua miradi ya mbalimbali ya Wananchi na chama kwa ujumla.
Sehemu ya wakazi wa Tunduru mjini  wakishangilia  jambo wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake mapema leo jioni kwenye uwanja wa Baraza la Iddi,Wilayani humo na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu.
Maeleoz yakitolewa namna ya Korosho zinavyochambuliwa mara baada ya kubanguliwa na mashine ya kisasa,ampapo zao hilo la biashara linalotegemewa na wakulima wa Wilaya ya Tunduru wamekuwa wakilalamikia suala la bei kuwa ndogo inayopangwa na Wanunuzi hali inayowapelekea Wakulima wa zao hilo kukata tamaa na maisha yao kuendelea kuwa duni siku hadi siku.
Msimamizi wa Kiwanda cha Korosho,Korosho Africa Ltd akifafanua namna ya Korosho zinavyobanguliwa kwa kutumia mashine za kisasa kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa ameambatana na ujumbe wake,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na  Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro,Kinana na Ujumbe wake wanamalizia ziara yao leo ndani ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma na kesho kuwasili ndani ya Wilaya ya Namtumbo kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo ya chama na wananchi sambamba na miradi.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro,akizungumza na akina mama wanaofanya kazi ya kuchambua Korosho ndani ya kiwanda cha Korosho Africa mapema leo mchana walipokwenda kutembelea kiwandani hapo na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa kiwandani hapo.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na akina mama wanaofanya kazii ya kuchambua Korosho ndani ya kiwanda cha Korosho Africa,ambao baadhi ya akina mama hao walilamika suala la ujira wanaolipwa kuwa ni mdogo na haukidhi mahitaji yao ya kila siku.
Uchambuzi wa Korosho ukiendelea.

KUTOKA MICHUZI
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger