Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana ukipita leo katika 'mkeka' wa barabara, ulipokuwa ukitokea wilayani Namtumbo kwenda wilayani Songea mkoani Ruvuma.Ndugu Kinana yuko katika ziara mkoani Ruvuma, kukagua utelekezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kushirikiana nao kupata njia za kuzitatua, barabara hiyo ni miongoni mwa barabara kadhaa zilizojengwa katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya CCM na kuwaondolea wananchi kero ya kusafiri kwenye barabara mbovu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki shughuli za ujenzi katika Zahanati ya Mahilo wilayani Songea mjini .
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba ya mwalimu kwenye shule ya sekondari Mdandamo wilayani Songea mjini
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua ujenzi wa nyumba ya maabara katika shule ya sekondari Mdandamo wilayani Songea mjini
Katibu wa NEC, Itikati na Uenezi Nape Nnauye akishirikiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wai Ruvuma, kuondosha gogo kwenye eneo la ujenzi wa Zahanati katika Kata ya Mahilo, Songea mkoani Ruvuma.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na waasisi wa CCM wilaya ya Songea mjini, kutoka kushoto ni Mzee Hashimu Gawaza na kulia kwa Katibu Mkuu ni Mzee Clemenci Nyoni ambao walikaa kikao cha kwanza na Mwalimu Nyerere tarehe 12 Agosti 1957 wakati wa harakati za kuikomboa nchi,anayefuatia kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndugu Oddo Mwisho.
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akiwa na Wazee hao.
Post a Comment