Mwili wa Mtanzania Jerry Isaack Mruma aliyekuwa akisoma Chuo
Kikuu cha Kimataifa cha Marekani (USIU) tawi la Nairobi nchini Kenya akichukua Shahada ya
Uzamili ya Utawala wa Biashara (MBA) aliuawa wakati akitoka kwenye hafla ya
usiku wa Mtanzania mjini Nairobi. Mwili
wake ulipatikana mwishoni mwa wiki iliyopita. Amezikwa leo katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Familia
ya Isaack Mruma ikiwa katika ibada maalum ya kumuombea marehemu
iliyofanyika katika Kanisa la KKKT, Usaharika wa Mbezi Beach Dar es
Salaam.
Kutoka
kushoto ni Mama mzazi wa Jerry, Bi Joyce Mruma, Khan Mruma ambaye ni
kaka wa marehemu, baba mzazi wa Jerry, Isaack Mruma na mdogo wake Kelvin
Mruma wakiwa katika ibada hiyo. PICHA ZAIDI FATHER KIDEVU BLOG
Post a Comment