Millen Happiness Magese (kulia) akikagua baadhi ya miradi
yake manispaa ya Mtwara.
Mwanamitindo wa
kimataifa wa Tanzania, Millen Happiness Magese amewataka watu binafsi na
makampuni mbalimbali kujitokeza kwa wingi katika kusaidia tasnia ya elimu hasa
katika maeneo yasiyopewa kipaumbele ili kuwaokoa watoto wa maeneo hayo
kutotumbukia katika vitendo visivyo vya kimaadili. Rai hiyo ameitoa wakati
alipotembelea miradi yake aliyoifadhili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na
utengenezaji wa madawati.
Millen Happiness Magese akiwa amepozi na wanafunzi huku
wakiwa wamekalia madawati aliyochangia katika shule hiyo.
Sehemu ya madawati yaliyotolewa na mrembo huyo katika
shule ya Msingi Mjimwema.
Millen akizidi kukagua miradi hiyo leo.
Ujenzi wa madarasa unaendelea katika shule ya msingi Mjimwema
iliyopo manispaa ya Mtwara ambapo mradi wa kutengeneza madawati ulikabidhiwa
kwa vikundi mbalimbali vya wajasiriamali mkoani hapo kwa mpango maalum kupitia
ofisi ya mkuu wa Wilaya, Mheshimiwa Wilman Ndile. Jumla ya madawati hamsini na
tano (55) yenye thamani ya shilingi milioni tano yalikuwa tayari
yameshatengenezwa kama walivyoahidi wajasiriamali hao wakati wakikabidhiwa kazi
ya utengenezaji wa madawati hayo.
Millen akiwa pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mjimwema
iliyopo manispaa ya Mtwara ambapo madarasa yanajengwa na pia pia aliwanunulia
wanafunzi hao madaftari kama waonekanavyo pichani.
Madawati hayo yalikabidhiwa rasmi na Millen yalikabidhiwa
kwa wanafunzi wa shule ya msingi Lilungu. Kwa upande wa afisa elimu wa manispaa
ya Mtwara Frola Aloys amewataka wadau wa elimu kuonesha uzalendo wa hali ya juu
kwa maeneo ya Kusini mwa Tanzania huku mkuu wa shule ya msingi Lilungu Abdul
Nangomwa akielezea changamoto zinazoendelea kuikumba sekta ya elimu katika
shule za msingi wilayani Mtwara.
Mbali na kukabidhi madawati Millen alipotembelea ujenzi
unaoendelea shule ya msingi Mjimwema na kutoa zawadi ya madaftari napenseli kwa
wanafunzi hao ambapo mpaka sasa shule in mikondo mitatu ambayo ni kuanzia
darasa la awali mpaka darasa la pili.
Ziara hiyo ya mrembo huyo aliyewahi kushika taji la Miss
Tanzania mwaka 2001, ni mwendelezo wa shughuli za kijamii anazozifanya nchini
Tanzania hasa katika kusaidia makundi yenye mahitaji maalumu na yale yasiyopewa
kipaumbele.
Mwanzoni mwa mwaka huu Millen Magese alitoa kiasi cha
shilingi milioni kumi na tano katika kusaidia huduma hiyo ya elimu katika
manispaa ya Mtwara.

Post a Comment