Home » » NBC YAIMWAGIA TAYOA MSAADA WA SHS MILIONI 100

NBC YAIMWAGIA TAYOA MSAADA WA SHS MILIONI 100

Written By JAK on Thursday, November 28, 2013 | 3:53 AM


 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu (kushoto) akipokea mfano wa hundi ya shs milioni 100 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Bi. Mizinga Melu kusaidia mradi wa mafunzo ya masuala ya ajira na ujasiriamali kwa vijana wa Shirika la kuelimisha vijana nchini (TAYOA). Hafla ilifanyika wakati wa tukio la uzinduzi wa mradi huo unaodhaminiwa na NBC jijini Dar es Salaam jana. Katikani ni Mkurugenzi Mkuu wa TAYOA, Peter Masika.
 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Bi. Mizinga Melu (katikati) na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Bi. Mwinda Kiula Mfugale wakionyesha vipeperushi kuashiria uzinduzi wa tovuti ya vijanatz.com ikiwa na habari kuhusu ajira (kazitz.com), fedha (fedhatz.com) na ujasiriamali (biasharatz.com). Hafla hiyo ilikwenda sambamba na uzinduzi wa mradi wa mafunzo ya masuala ya ajira na ujasiriamali kwa vijana  wa Shirika la kuelimisha vijana nchini (TAYOA) unaodhaminiwa na NBC.
3: Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu akishikana mikono na Mkurugenzi Mkuu wa TAYOA, Peter Masika baada ya kukabidhi  mfano wa hundi ya shs milioni 100 zilitotolewa na benki hiyo kusaidia mradi wa mafunzo ya masuala ya ajira na ujasiriamali kwa vijana wa Shirika la kuelimisha vijana nchini (TAYOA). Hafla ilifanyika wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi huo unaodhaminiwa na NBC. Kushoto ni Naibu Waziri wa Maendeleo aya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu na kulia ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Mwinda Kiula Mfugale.
 Mkurugenzi Mkuu wa TAYOA, Peter Masika (kushoto), Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia), na Meneja Mkuu wa Mawasiliano wa NBC, William Kallaghe wakibadilishana mawazo katika hafla hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa TAYOA, Peter Masika (kushoto), Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia), na Meneja Mkuu wa Mawasiliano wa NBC, William Kallaghe wakibadilishana mawazo katika hafla hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Mizinga Melu akizungumza na vijana na wageni wengine kuhusu huduma za kibenki na kuhusu mikakati ya benki kusaidia suala la ajira na ujasiriamali kwa vijana katika hafla hiyo.
Wasanii wakitoa burudani kusindikiza uzinduzi wa mradi wa mafunzo ya masuala ya ajira na ujasiriamali kwa vijana wa Shirika la kuelimisha vijana nchini (TAYOA) unaodhaminiwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) jijini Dar es Salaam
NA MICHUZI BLOG
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger