Home » » TAMKO LA KUJIUZULU MAKAMU MWENYEKITI (BARA) WA CHADEMA

TAMKO LA KUJIUZULU MAKAMU MWENYEKITI (BARA) WA CHADEMA

Written By JAK on Sunday, November 24, 2013 | 7:23 PM


Said A. Arfi (MB)
Salaam,
Napenda kuwasilisha kwako (Mwenyekiti Taifa CHADEMA) taarifa ya kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara kuanzia Leo Ijumaa 22 Novemba 2013 kwa kuchoshwa na Unafiki unaoendelea ndani ya Chama. Napenda ifahamike pia kwangu maslahi ya Wapiga kura, Wakaazi na wananchi wa Mpanda Mjini na Wilaya ya Mpanda ni muhimu katika kuwatumikia, hivyo basi sipo tayari kuchaguliwa marafiki. 


Kwa kipindi kirefu zimekuwepo shutma dhidi yangu na kutiliwa mashaka mahusiano yangu na Mhe Pinda Waziri Mkuu. Pamoja na kulijadili katika vikao kadha Mpanda na Dar es Salaam bado yapo mashaka kwa nini alipita bila kupingwa hayo yalikua maamuzi ya Wanampanda kwenu imekua ni tatizo lakin hamsemi kwa nini Majimbo mengine 16 nchini yalipita bila kupingwa mlikua wapi na nani alaaumiwe huu ni Unafiki  wa kupindukia.



Aidha mmechukizwa sana kwa nini nilihoji kauli ya Muasisi wa Chama Mhe Mtei kutuchagulia viongozi naomba ifahamike wazi kwamba huu ni mtazamo wangu na utabakia hivyo siku zote kwa chama cha demokrasia kutoruhusu uongozi wa kiimla kwa kukidhi matakwa ya Waasisi ambao huvigeuza vyama kuwa Mali binafsi.
Kwa kusema ukweli na kusimamia ukweli daima itabakia kuwa lengo langu katika maisha yangu siku zote hata kama itanigharimu maisha yangu



Nawasilisha.
Said A. Arfi (MB)
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger