Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akitoa hotuba yake kwa Askari
na Maofisa wa Jeshi la Polisi, Viongozi wa Mashirika na Taasisi zisizo za Serikali pamoja
na wakazi wa Temeke kabla ya kuzindua Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa Kuboresha
Madawati ya Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi. Tukio hilo lilifanyika Kituo cha Polisi
Chang’ombe, Temeke jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP)
Said Mwema. Waziri Nchimbi akatika hotuba yake alilishukuru Jeshi la Polisi pamoja na
Viongozi wa Mashirika na Taasisi zisizo za Serikali kwa kusaidia masuala ya kupambana na
unyanyasaji wa kijinsia nchini.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akikionyesha kitabu cha Mpango
Mkakati wa miaka mitatu wa kuboresha madawati ya Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi
katika uzinduzi uliofanyika Kituo cha Polisi Chang’ombe, Temeke jijini Dar es Salaam leo.
Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema, wapili kushoto ni Balozi wa Umoja
wa Ulaya nchini, Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi na Kushoto ni Kamanda wa Polisi, Kanda
Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova. Waziri Nchimbi akatika hotuba yake alilishukuru
Jeshi la Polisi pamoja na Viongozi wa Mashirika na Taasisi zisizo za Serikali kwa kusaidia
masuala ya kupambana na unyanyasaji wa kijinsia nchini.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akikata utepe kuzindua ofisi ya
Dawati la Jinsia na Watoto katika Mkoa wa Kipolisi Temeke. Kushoto ni Balozi wa Umoja wa
Ulaya nchini, Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi na Kushoto ni Kamanda wa Polisi, Kanda
Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova. Waziri Nchimbi akatika hotuba yake alilishukuru
Jeshi la Polisi pamoja na Viongozi wa Mashirika na Taasisi zisizo za Serikali kwa kusaidia
masuala ya kupambana na unyanyasaji wa kijinsia nchini. Picha zote na Felix Mwagara,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Post a Comment