Home » » Aliyowasilisha Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo kwenye kongamano la rasilimali na madini UDASA

Aliyowasilisha Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo kwenye kongamano la rasilimali na madini UDASA

Written By JAK on Thursday, December 12, 2013 | 3:10 AM


Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akisisitiza jambo kwa Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Ubou Sabaa (aliyeketi upande wa kulia).
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi akitoa maelezo  juu ya maendeleo ya sekta ya nishati kwa Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Ubou Sabaa (aliyeketi upande wa kulia). Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kuwasilisha taarifa ya maendeleo ya sekta ya nishati katika maeneo ya ulipaji kodi, mapato,  ujenzi wa bomba la gesi ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa shirika la Tanesco
Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) Ubou Sabaa akizungumza katika kikao hicho. Makamu huyo aliambatana na ujumbe wake ambapo alifurahishwa na  kasi ya ukuaji  wa sekta ya nishati na kuahidi kutoa ushirikiano wa kutosha pale itakapohitajika



==============  ==========  ============
Mwishoni mwa wiki Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo alialikwa kwenye kongamano lililojadili  rasilimali za taifa ikiwa ni pamoja na ushirikishwaji wa wananchi lililofanyika katika  ukumbi wa Nkuruma, chuo kikuu cha Dar es Salaam. Kongamano hilo lilihusisha wadau wengine ikiwa ni pamoja na Mbunge wa Ubungo (Chadema) John Mnyika, Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dkt Reginald Mengi na wadau wengine.

Nawasilisha presentation  za Mhe. Waziri kwa ajili ya kuhabarisha umma. Pia nimeambatisha na video iliyowasilishwa siku ya kongamano hilo.

Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger