Home » » Balozi Seif Ali Idd apokea mchango wa sh. Mil. 15 kutoka kwa mwenyekiti wa Yanga,Yussuf Manji

Balozi Seif Ali Idd apokea mchango wa sh. Mil. 15 kutoka kwa mwenyekiti wa Yanga,Yussuf Manji

Written By JAK on Friday, December 20, 2013 | 9:24 PM


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ambae pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya maadhimisho ya Kitaifa akipokea fedha taslim Shilingi Milioni 15,000,000/- kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Quality Group Bwana Yussuf Manji kuchangia sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia miaka 50.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Quality Group ambae pia ni Mwenyekiti wa Kalabu ya Soka ya Yanga ya Dar es salaam Bwana Yussuf Manji mara baada ya kupokea mchango wa mfanyabiasra huyo nyumbani kwake Mazizini Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa (Zanzibar) amepokea mchango wa fedha kutoka  kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Quality Group ambae pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya soka ya Yanga ya Dar es salaam Bwana Yussuf Manji ili kusaidia kuchangia sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia miaka 50.

Bwana Manji ambae alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ushiriki wa Timu yake ya Yanga katika mashindano ya Mapinduzi Cup alikabidhi mchango huo nyumbani kwa Balozi Seif Mazizini nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Alisema Kampuni yake pamoja na Timu yake imehamasika kutoa mchango huo wa Shilingi Milioni  Kumi na Tano { 15,000,000/- } kufuatia umuhimu wa Tanzania  kukabiliwa na sherehe hizo kubwa  za maadhimisho ya Nusu karne ya mapinduzi ya Zanzibar.

Akipokea mchango huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alimpongeza  Bwana Yussuf Manji kwa uamuzi wa Taasisi zake kuona umuhimu wa kusaidia sherehe hizo zilizokabiliwa na masuala mengi kutokana na umuhimu wake kihistoria.

Balozi Seif alimuhakikishia Kiongozi  huyo wa Quality Group na Timu ya Soka ya Yanga pamoja na wananchi wote kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano iko katika utaratibu wa kukamilisha maandalizi ya mwisho ya maadhimisho hayo.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

20/12/2013.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger