- *Yasema itatafakari na kuamua ipasavyo hoja za Tume
- *Yasisitiza mchakato utumike kuwaunganisha Watanzania
Chama Cha Mapinduzi kimeipongeza Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini kwa kazi iliyofanya kuufikisha mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya hapa ulipofika. Akizungumza katika mahojiano maalumu na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya Tume kuwasilisha rasimu ya pili ya katiba Nape alisema;
“CCM inaipongeza Tume kwa kazi waliofanya, tunatambua kazi kubwa waliyofanya, wamekamilisha kazi waliyotumwa salama na kwa wakati. Sasa tuwaachie wanaondelea na mchakato yaani bunge la katiba na hatimaye wananchi. Tunautakia kila lakheri mchakato huu, utumike kutuunganisha watanzania badala ya kutugawa” amesema Nape.
Kuhusu pendekezo la Tume la muundo wa Muungano wa serikali tatu Nape anasema; “Tumesikiliza hoja za tume juu ya sababu za kuendelea kupendekeza muundo wa serikali tatu, tumezisikia, tutazichukua,kuzipeleka kwenye vikao vya Chama baada ya tafakuri ya kutosha tutaamua ipasavyo” alisisitiza Nape.Aidha Nape alitumia nafasi hiyo kuwatakia watanzania kila lakheri kwenye mwaka mpya wa 2014.
Post a Comment