Home » » HITMA YA MOHAMMED GHAZA ILIYOFANYIKA NORTH CAROLINA

HITMA YA MOHAMMED GHAZA ILIYOFANYIKA NORTH CAROLINA

Written By JAK on Tuesday, December 31, 2013 | 6:27 AM


 Jana siku ya jumapili Dec 29, 2013 ndio kulifanyika hitma ya Marehemu Mohammed Omar Ghaza aliyetutoka tarehe 23 mwezi wa December waka 2013.
Hitma ilifanyika Durham, NC .
Nassor , Eddy, Yafidh, Amani na wengineo wakitia Fatha kabla ya kuomba Dua.
Watanzania na marafiki zao wakijumuika pamoja kwenye hitma ya Mohammed Ghaza iliyofanyika Durham, North Carolina nchini Marekani Jumapili ya Dec 29, 2013.
Hitma ya marehemu Mohammed Ghaza aliyefariki kwa ajali ya gari mapema asubuhi ya Dec 23, 2013 kwenye makutano ya Martin Luther King Jr. Boulevard na Elm Eugene Street. Marehemu alikuwa na mchumba wake Christa aliyekuwa akiendesha Ford Focus ya mwaka 2001 akielekea mashariki na marehemu akiwa abiria gari ilipoteza muelekeo na kutoka nje ya barabara na iliporudi ikagongwa na trela ya trekta iliyokua ikiendeshwa na Rodney Morris Marehemu alikimbizwa hospitali ya Moses Cone na kufariki baadae kutokana na majereha aliyopata. Christa anaendelea vizuri.
Watanzania na marafiki zao wakijumuika pamoja kwenye hitma ya Mohammed Omar Ghaza iliyofanyika Durham, North Carolina nchini Marekani siku ya Jumapili Dec 29, 2013.
Watanzania na marafiki zao wakijumuika pamoja kwenye hitma ya Mohammed Omar Ghaza iliyofanyika Durham, North Carolina.
wakati wa kupata makulaji
Ndugu jamaa na marafiki wakipata sunna ya chakula.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger