
Kinana akimkabidhi Mwenyekiti wa Vijana wa Tarafa ya Ikuwo, Tunsume Shemgogo ufunguo ikiwa ni ishara ya kukabidhi Trekta kwa vijana wa Mkoa wa Njombe kwa ajili ya kusaidia Kilimo.Trekta hilo limetolewa na CCM kwa vijana wa mkoa huo,aidha makabidhiano hayo yamefanyika leo kwenye kambi ya vijana iliyopo kweneye kijiji cha Mlengu,kata ya Kiangala,tarafa ya Ikuwo wilayani Makete,mkoani Njombe,ambapo kambi hiyo ina eneo la ekari 300 za mashamba,Ndugu Kinana aliahidi kutoa Trekta hilo wakati alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo mnamo Agosti mwaka huu,baada ya kuelezwa jinsi vijana hao walivyojiunga pamoja katika kikundi na kuamua kujishughulisha na kilimo ili kujikwamua na suala zima la umaskini.
Kinana akilima shamba la vijana wa Tarafa ya Ikuwo kwa kutumia trekta wakati wa makabidhiano yaliyofanyika katika Kijiji cha Mlengo, wilayani Makete mkoani Njombe leo jioni.shamba
hilo la Vijana
wapatao 252 wakiwa na shamba lenye ukubwa wa ekari 300,wamekabidhiwa Trekta lenye thamani ya sh. mil 42.
wapatao 252 wakiwa na shamba lenye ukubwa wa ekari 300,wamekabidhiwa Trekta lenye thamani ya sh. mil 42.
Kinana (kulia), Dk. Asha Rose Migiro wakiangalia vyerehani vya kisasa walipotembelea Chuo cha Ufundi Stadi cha Makete-VETA.
Injinia Asifiwe Swalo akielezea mashine mojawapo ya mbao inayofanya kazi ya kuchana mbao katika mianguko mbalimbali ikiwemo na kuweka urembo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake mara baada ya kutembelea karakana ya ufundi Selemara.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki kupanda mti nje ya eneo la chuo hicho cha VETA,kushoto kwake anaeshuhudia ni Mkurugenzi wa VETA nyanda za juu kusini,Bi.Monica Mbele.
Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt.Asharose Migiro akishiriki upandaji miti nje ya eneo la chuo hicho cha VETA,mapema leo Wilayani Makete mkoani Njombe.
Pichani katini katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt.Asharose Migiro akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Makete,Mh. Josephine Matiro (kushoto) na Mkurugenzi wa VETA nyanda za juu kusini,Bi.Monica Mbele.
Post a Comment