Habari zimetujia sasa hivi zinasema abiria kadhaa akiwemo Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa wamenusurika kifo, baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kuwa pasuka matairi yote manne ya nyuma wakati ilipokuwa ikitua katika uwanja wa Arusha leo mchana.
Ndege hiyo ya shirika la ndege la precision aina ya ATR ilipata ajali hiyo wakati ikitua, ambapo Matairi yote manne ya nyuma yalipasuka na kusababisha taharuki kubwa kwa abiria. Ila hakuna mtu aliyedhurika katika ajali hiyo.
"Yaani Mungu ni mkubwa kwa kweli, ametunusuru maisha yetu na kiongozi kipenzi chetu Lowassa...Mungu atamlinda jamani...siamini" alisikika akisema mama mmoja miongoni mwa abiria hao wakati akishuka.
Post a Comment