Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Bi.
Irene Isaka akipokea tuzo ya NBAA toka
kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Mh. Goodluck Ole- Medeye
baada ya kuwa
mshindi wa kwanza katika uwasilishaji wa hesabu safi katika mwaka 2012,katika kundi la Mamlaka za
Usimamizi zinazotumia mfumo wa “ International Public Sector Accounting
Standards ( IPSAS) katika uandaaji wa mahesabu wakati wa hafla ya utoaji tuzo za NBAA iliyofanyika katika hotel ya Naura Spring Arusha.
Mwenyekiti wa Bodi wa NBAA Professor Musa
Assad akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa
SSRA Bi. Irene Isaka wakati wa hafla ya utoaji tuzo za NBAA iliyofanyika katika hotel ya Naura Spring Arusha.
Mjumbe wa bodi ya NBAA na Mkurugenzi wa zamani wa bodi
ya SSRA bwana Juma Muhimbi akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa SSRA Bi.Irene Isaka mara
baada ya kupokea tuzo ya NBAA, nyuma yake
Mkaguzi wa ndani wa SSRA Bwana.
Peter Mbelwa.
Mkurugenzi wa Uandikishaji na matekelezo Bi. Lightness Mauki (kushoto) na wageni wengine wakisikiliza maelezo yanayotolewa na Mkurugenzi mkuu wa NBAA bwana Pius Maneno ( hayupo pichani) wakati wa halfa ya utoaji tuzo ya NBAA wakati wa hafla ya utoaji tuzo za NBAA iliyofanyika katika hotel ya Naura Spring Arusha.
Picha ya pamoja ya washindi wote wa kwanza wa tuzo ya NBAA.
Mkurugenzi wa Fedha Utawala na Mipango Bwana. Mohamed Nyasama na Bi. Sarah Kibonde Msika Mkuu wa mawasiliano na uhamasishaji wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa SSRA Bi. Irene Isaka na mara baada ya kupokea tuzo ya NBAA katika hotel ya Naura Spring –jijini Arusha.
Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa SSRA mara baada ya kupokea tuzo ya NBAA wakiwa wshindi wa kwanza katika uwasilishaji wa mahesabu safi kwa kutumia mfumo wa IPSAS, wa pili kutoka kushoto ni bwana Athumani Juma – Mhasibu wa SSRA.
Mkurugenzi Mkuu wa SSRA Bi Irene Isaka akiongea na waandishi wa habari kuhusu tuzo ambayo ya NBAA ambayo SSRA wameipata wakiwa washindi wa kwanza .
Post a Comment