Home » » Moto wawaka bungeni - KAGASHEKI AJIONDOA, Nchimbi, Nahodha na Mathayo waenguliwa

Moto wawaka bungeni - KAGASHEKI AJIONDOA, Nchimbi, Nahodha na Mathayo waenguliwa

Written By JAK on Friday, December 20, 2013 | 10:34 PM


Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamisi  Kagasheki amejiuzulu wadhifa wake baada ya mjadala mkali wa Bungeni mjini Dodoma hivi sasa. Habari zaidi kwa kirefu zitakuja baadaye.
Hii inatokana na Operesheni Tokomeza iliyolenga kuondoa ujangili uliokithiri nchini. 
Tangu kuanza kwa operesheni hiyo, kumekuwa na malalamiko mbalimbali kutoka kwa wabunge, wanaharakati na wananchi dhidi ya askari waliokuwa wakiiendesha yakiwamo ya watu kujeruhiwa, kuchomewa nyumba, mifugo kuuawa, kupigwa na uporaji.
Operesheni hiyo ilikuwa ikiendeshwa kwa pamoja na askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Polisi, Usalama wa Taifa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa).
Operesheni hiyo ilizuiwa baada ya suala hilo kutinga bungeni na watunga sheria hao kuweka kando tofauti zao za kiitikadi na kuungana wakitaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki na Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Mathayo David Mathayo wawajibike.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Dk David Mathayo David, akitoa utetezi wake, akidai kuwa ameonewa.
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda ametaka uthibitisho usio na shaka kwa waliohusika wote na taasisi zao kuchunguzwa kiundani ili hatua stahiki zichukuliwe. Kuendelea kulinda rasilimali na hifadhi za Taifa amekutaja kuwa ni  muhimu. Pia amesema ameongea na Waziri mmoja mmoja kuwa ni busara ushauri wa wabunge utekelezwe. Amebainisha kuwa hata baada ya kuongea na Rais, Mkuu wa nchi huyo ameridhia tume iundwe na kila aliyehusika awajibike.
Amesema Rais ameshauri
 kutengua uteuzi wa mawaziri wote wanne ( Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Shamsi Vuai Nahodha, Wazir wa Mambo ya Ndani Dkt Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt David Mathayo, na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamisi Kagasheki) kama ambavyo wabunge walivyopendekeza.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe  James Lembeli (pichani juu) amesema kuwa kamati yake imeridhishwa na matokeo ya ripoti ya kamati iliyosababisha hayo yote, na kwamba maelezo ya taarifa ya kamati kimsingi yote yamekubalika.
Kuhusu kumhusisha Dkt Mathayo ni kuwa  Rais alishatoa maagizo tisa miongoni likiwepo swala la kushughulikia wafugaji wanaohamahama. Amesema pia Rais aliagiza pia kuwa wafugai wawe wa kisasa, pia kutafuta missing link ya mifugo isipotee na pia kutafuta masoko nje ya nchi, ambapo amesema mengi hayajatekelezwa.
Ameweka bayana kuwa chimbuko kubwa ni Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, na kwamba Waziri hakuwa anapewa taarifa za mara kwa mara.
Ameomba kipengele kiongezwe kuwa Katibu mkuu na watendaji wake wakuu  waliohusika kuandaa Mpango kazi wa 'Operesheni Tokomeza' wawajibishwe.
Amesema rushwa iliyoko ndani ya wizara ya Maliasili na Utalii inatisha.
Spika amuomba Mwanasheria mkuu kutumia kifungu kuongeza muda. Naye ameomba  kuundwa tume ya kisheria ya mahakama.
Spika Mhe. Anne Makinda ameahirisha Bunge (saa tatu na dakika nne usiku huu) hadi saa tatu kesho asubuhi. 

 Juu ni Dkt Emmanuel Nchimbi na chini ni Mhe Shamsa Vuai Nahodha
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger