Mwanamzuki mwimbaji wa Kimataifa wa nyimbo za Kiroho a.k.a Injili kutoka nchini Afrika Kusini,Solly Mahlangu pichani kati akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwal J.K.Nyere jijini Dar jioni ya leo.Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa tamasha la krisimasi,Bwa.Alex Msama na wadau wengine waliofika kumlaki mwanamuziki huyo mahiri anaetarajiwa kutumbuiza hapo kesho kwenye uwanja wa Taifa wakati wa tamasha la krisimasi.
Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions Ltd,inayoandaa tamasha la Krisimasi,Bwa.Alex Msama akizungumza na baadhi ya Wanahabari kuhusiana na ujio wa mwanamuziki wa Afrika Kusini,Solly Mahlangu aliyewasili jioni ya leo jijini Dar tayari kuungana na wanamuziki wengine wa nyimbo ya Injili kwa ajili ya kutumbuiza hapo kesho kwenye tamasha la Krisimasi,ambalo linasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wake.
Mwanamuziki wa nyimbo za Injili,Solly Mahlangu akiwapungia mikono mashabiki wake waliofika kumlaki mara baada ya kuwasili jioni ya leo kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwal J.K.Nyere jijini Dar jioni .Kulia kwake ni Mwenyekiti wa tamasha la krisimasi,Bwa.Alex Msama na wadau wengine waliofika kumlaki mwanamuziki huyo mahiri anaetarajiwa kutumbuiza hapo kesho kwenye uwanja wa Taifa wakati wa tamasha la krisimasi.
Post a Comment