Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki Moon akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwaajili ya kufanya mazungumzo nae.
 |
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki Moon
akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwenye ofisi yake iliyopo Makao Makuu
ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani jana |
 |
Bwana Ban Ki Moon na Rais Mrisho Kikwete wakijadili jambo ambapo masuala mbalimbali ya kimataifa hususan masuala ya amani na ushiriki
wa majeshi ya Tanzania katika kudumisha amani sehemu mbalimbali Afrika na
katika nchi nyingine duniani yalijadiliwa, ambapo Tanzania ikiwa ina majeshi ya kulinda amani katika nchi
kadhaa ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Darfur nchini Sudan na
Lebanon.
Rais Kikwete yupo jijini New York nchini Marekani ambapo anaendelea
vyema na ukaguzi wa kawaida wa afya yake. |
 |
Bwana Ban Ki Moon na Rais Mrisho Kikwete wakiwa katika picha ya pamoja |
(Picha na Freddy Maro)
Post a Comment