Home » » Rais Kikwete atunuku Kamisheni Maofisa wa Jeshi la Wananchi Monduli ,Mkoani Arusha

Rais Kikwete atunuku Kamisheni Maofisa wa Jeshi la Wananchi Monduli ,Mkoani Arusha

Written By JAK on Monday, December 16, 2013 | 5:27 AM


Amiri Jeshi Mkuu ,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi Luteni usu Evarist Mawalla wakati alipowatunuku Kamisheni maofisa wapya wa Jeshi la Wananchi Tanzania baada ya kuhitimu mafunzo yao katika Chuo Cha Jeshi Monduli Juu mjini Arusha jana.Luteni Usu Mawalla aliibuka mwanafunzi bora katika mafunzo hayo yaliyochukua takribani mwaka mmoja ambapo wanafunzi kutoka nchi za kigeni pia walishiriki.
Amiri Jeshi Mkuu ,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi Luteni Usu Immaculata Leodgar Mapunda baada ya kuibuka mwanafunzi bora wa kike katika kozi ya maafiseshi la Wananchi wa Tanzania iliyofanyika Chuo Cha Jeshi Monduli mjini Arusha jana.Katika mafunzo hayo yaliyochukua takriban mwaka mmoja baadhi ya wanafunzi kutoka nchi za kigeni nao walishiriki mafunzo hayo.
Amiri Jeshi Mkuu ,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa hafla ya kuwatunuku Kamisheni Maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania iliyofanyika Chuo Cha Jeshi Monduli mjini Arusha jana.Katika mafunzo hayo yaliyochukua takriban mwaka mmoja baadhi ya wanafunzi kutoka nchi za kigeni nao walishiriki mafunzo hayo.(picha na Freddy Maro)
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa pole na kumrekebisha tai mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa ambaye juzi alinusurika katika ajali ya ndege baada ya ndege aliyokuwa akisafiria inayomilikiwa na Shirika la Ndege ya Precision kupasuka matairi yote ya nyuma wakati ikitua katika uwanja wa ndege wa mjini Arusha. Rais Kikwete alikuwa Monduli Mkoani Arusha kutunuku kamisheni kwa maafisa wapya wa jeshi la Wananchi wa Tanzania katika chuo cha jeshi Monduli.


Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger