Kwa Niaba ya CCM Tawi la Uingereza tunapenda kuungana na Wanachama,
Wapenzi na waTanzania wote kwa ujumla katika kusherehekea sikukuu
za Krismas na Ujio wa Mwaka Mpya wa 2014.
Uingereza sherehe hizi zimetukuta katika hali ya hewa yenye
kimbunga kingi na mvua nyingi zisizoisha, na hivyo kuathiri maandalizi kwa namna moja au nyingine kutokana na vizuizi katika baadhi ya
miundo mbinu hasa barabara na reli.
Aidha, kama inavyojulikana Ulimwenguni Ukata wa kifedha nao umeshika
hatamu. Kuyumba kwa Uchumi wa Nchi nyingi kubwa na ndogo na kuyumba
kumepelekea mfumuko wa bei za bidhaa hasa vyakula . Tatizo ambalo
limeukumba ulimwengu mzima.
Licha ya vikwazo hivi na vingine ,hatuna budi kumaliza mwaka kwa kuangalia nyuma na kuona yale mengi yaliyofanikishwa. Kwa hali hii ,
CCM UK tunachukua nafasi hii kuipongeza kwa dhati Serikali ya awamu ya
nne ya Jamahuri ya Muungano ya Tanzania kwa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM.
Mfano ulio wazi ni katika miundo mbinu ya barabara ambapo asilimia
kubwa ya Nchi sasa inaunganika kwa barabara na maeneo mengi sasa yanafikika kirahisi kwa barabara,ambazo nyingi zimejengwa kwa kiwango cha lami. Hii imesaidia sana kupeleka mahitaji muhimu vjijini na uvutiaji katika uwekezaji, na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi wa Tanzania.
Tunapenda kuwasihi WaTanzania wenzetu , tutumie kipindi hiki cha
mapumziko ni vyema pia kutafakari na kupongeza yale mazuri yaliyofanywa na serikali na vilevile kuungana pamoja na kuchangia katika kuleta Maendeleo ya
Mtanzania na si kubeza juhudi za maendeleo kwa sababu ya tofauti za
kiitikadi na za kisiasa .
Ni muhimu kwanza tujipongeze wenyewe kama watanzania kwa nafasi pekee
tuliyonayo na tunayojivunia ya amani ya nchi yetu. Tusikubali kurubuniwa
kwa namna au hali ya aina yeyote na hasa inapobidi tujiulize na
kutafakari ni nini kinatufanya watanzania tukawa wamoja , vilevile kudumisha Amani, Umoja na Upendo wetu.
WaTanzania hatuna budi kulinda amani ya nchi yetu na upendo miongoni
mwetu kwa gharama yeyote ile na bila kuyumbishwa au kutetereka ili tuweze kuachia vizazi vyetu vijavyo Urithi ulio mwema kuliko wowote Ule. TANZANIA yenye Amani, Upendo na Utulivu.
"MUNGU IBARIKI TANZANIA"
Post a Comment