Waziri
wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akiongea na wafanyakazi wa Wizara na Wakuu
wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo leo jioni katika mkutano maalum wa
kufunga mwaka na kuwakaribisha rasmi Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Shaaban
Mwinjaka(kulia kwa Waziri Mwakyembe)na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mrs
Monica Mwamunyange(kushoto kwa Waziri Mwakyembe Katika ukumbi wa Karimjee,jijini
Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mrs
Monica Mwamunyange akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa kufunga mwaka na
kuwakaribisha rasmi Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu huyo. Mkutano huo
umefanyika leo jioni katika ukumbi Karimjee jijjini Dar es Salaam. Aidha Naibu
Katibu Mkuu huyo amesisitiza ushirikiano na kujiwekea malengo katika utendaji kazi
wa kila siku.
Sehemu ya Watendaji wakuu wa taasisi zilizo
chini ya Wizara ya Uchukuzi na wafanyakazi wa Wizara hiyo wakimsikiliza kwa
makini Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk. Shaaban Mwinjaka(Hayupo pichani) wakati
wa mkutano maalum wa kufunga mwaka na kuwatambulisha rasmi viongozi hao uliofanyika
katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe (wa
tano kutoka kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu, Dk. Shaaban
Mwinjaka (wa tano kutoka kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mrs
Monica Mwamunyange (wa nne kutoka kushoto) na Watendaji wakuu wa taasisi zilizo
chini ya Wizara ya Uchukuzi leo alipokutana nao ili kuwatambulisha rasmi viongozi
hao kwa Watendaji Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Uchukuzi na
watumishi.
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akiwa
katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Shaaban Mwinjaka(wa
kwanza kulia mstari wa kwanza), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mrs Monica
Mwamunyange(wa pili kutoka kushoto mstari wa kwanza) na wakuu wa Idara na Vitengo
wa Wizara ya Uchukuzi leo jioni katika Mkutano maalum wa Waziri wa Uchukuzi
kuwatambulisha rasmi viongozi hao kwa Wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara
pamoja na Wafanyakazi wa WIzara hiyo.
Waziri wa Uchukuzi, Dk.
Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,
Dk. Shaaban Mwinjaka(wa tatu kutoka kulia mstario wa kwanza), Naibu Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo, Mrs Monica Mwamunyange (wa pili kutoka kushoto mstari wa
kwanza) na baadhi ya watumishi wa Wizara
ya Uchukuzi leo jioni katika Mkutano maalum wa Waziri wa Uchukuzi kuwatambulisha
rasmi viongozi hao kwa Wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara pamoja na
Wafanyakazi wa Wizara hiyo. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini Uchukuzi)
Post a Comment