Home » » BURIANI TONNY BARETTO

BURIANI TONNY BARETTO

Written By JAK on Monday, January 6, 2014 | 6:35 AM



Familia, ndugu, jamaa na marafiki asubuhi leo wamememiminika katika ukumbi wa Diamond Jubilee hall jijini Dar es salaam kutoa heshima zamwisho kwa  mwili wa Tonny Baretto. kabla ya kuelekea mazikoni katika Kijitonyama Crematorium, jijini Dar es salaam, ambako mwili wake utachomwa moto kama alivyousia kabla ya kuaga dunia.

 Marehemu alikuwa ni mmoja wa wanataaluma wa habari wakongwe aliyewahi kufanya kazi Tanzania Standard Newspapers (TSN) IPP Media na sehemu mbalimbali katika vitengo vya matangazo. Marehemu Baretto alifariki ghafla December 31, 2013 na kustua kila mtu.


 Mtoto wa marehemu John-Paul Baretto akisema machache kuhusu baba yake
 Mzee Ulli Mwambulukutu aliyepata kufanya kazi na marehemu akiwa Mhariri Mtendaji wa Daily News Enzi hizo akiongea machache
 Gabby Mgaya kutoka Daily News akimkumbuka Tonny
 Bosi wa ITV Joyce Mhavile akisema machache kuhusu Tonny Baretto
 Mjane wa marehemu Tonny Baretto, Pearl (wa pili kulia), watoto John Paul (kushoto) na Catherine Rose (kulia) na bibi yao, mama wa Pearl.
 Waombolezaji wakiifariji familia
 Mama Rose Mwapachu na Balozi Mwapachu wakiwafariji wafiwa
 John Paul akipewa pole na wadau
 Poles sana John Paul...
 Pole John....
 Pole sana kijana wetu....








 Ankal akiwa na marafiki wa karibu wa Tonny Baretto. Toka shoto ni Sukhdev Chatbar toka Arusha, Mukesh Josh, Ankal na Mkurugenzi wa Radio One Deo RWeyunga
Marafiki wa karibu wa Tonny Baretto wakisherehekea maisha ya marehemu.
Source Matukio Michuzi
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger