Home » » DUHHH!!!!!!! CHADEMA WACHAPANA MAKONDE WAKATI WA KESI YA ZITTO KABWE MAHAKAMANI DAR.

DUHHH!!!!!!! CHADEMA WACHAPANA MAKONDE WAKATI WA KESI YA ZITTO KABWE MAHAKAMANI DAR.

Written By JAK on Saturday, January 4, 2014 | 6:27 AM


Dar es Salaam,Tanzania

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imeahirisha kutoa hukumu ya kesi iliyofunguliwa jana na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Zuberi Kabwe (Chadema), kuhusu ombi la kuitaka Mahakama hiyo kuizuia Kamati Kuu ya Chama hicho, kutomjadili katika kikao ambacho kilipangwa kufanyika leo jijini Dar es Salaam.




Wanachama wa Chadema, wakitwangana nje ya Mahakama Kuu, jijini Dar es Salaam. 

Jaji John Utumwa alisitisha kutoa hukumu hiyo mpaka siku ya Jumatatu saa 4:00 asubuhi.Hata hiyo baada ya Jaji huyo kuahirisha kesi hiyo, nje ya Mahakama hiyo kulikuwa na vurugu kubwa baada ya kundi linalo unga mkono maamuzi ya Chadema kutwangana na kundi linalo muunga Zitto Kabwe.

 

Mwanachama wa Chadema, anayepinga hoja za Zitto Kabwe, akimtwanga mfuasi wa Zitto Kabwe. 

Hatua hiyo ilisababisha Askari wa Jeshi la Polisi kuingilia kati, huku wakiungana na upande wa Chadema na kuwatwanga marundi wafuasi wa Zitto waliokuwa na mambango kama ilivyokuwa kwa wenzao wa Chadema.

Kesi hiyo ilifunguliwa jana na wakili wa Mbunge huyo Albert Msando huku wakili wa Chadema Tundu Lissu akiweka pingamizi,hata hivyo Jaji John Utumwa wa Mahakama hiyo alitupilia mbali mapingamizi yote yaliyowekwa na Tundu Lissu,

Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger