Home » » HOJA YA HAJA: UTHIBITI WA MAGARI MAZITO BARABARANI UENDELEE KUOKOA MIUNDOMBINU YETU

HOJA YA HAJA: UTHIBITI WA MAGARI MAZITO BARABARANI UENDELEE KUOKOA MIUNDOMBINU YETU

Written By JAK on Saturday, January 4, 2014 | 5:58 AM


Kwa watu wote wanaoitakia mema nchi yetu, 
Naandika hii nikiwa na hasira iliyochanganyika na majonzi. Yaani hata sijui nianzie wapi. Awali ya yote naomba urudishe ukurasa wa kwanza zile picha za uharibifu wa barabara ulizoposti majuzi. 

Mimi niko hapa Sao Paulo huku Brazil. Nilistushwa sana sana na picha hizo pamoja na maelezo yake, kadhalika na maoni ya wadau wako. Ni dhahiri wengi ya wadau wako aidha ni kuendeleza tu tabia ya kubeza na kuponda kila kilicho mbele yao ama ni kwa sababu hawana habari ya kinachoendelea. 
Katika research niliyofanya katika mitandao ya kijamii na ya magazeti juu ya swala hilo, nimejikuta nafikia mahali kuamini kuwa swala hili halina tofauti na lile la Operesheni Tokomeza, ambapo mawaziri wane wamemwaga unga hivi hivi kiutani utani, japo hawahusiki moja kwa moja. Hii inaitwa uwajibikaji. 

Siku chache baadaye nimesoma Wizara ya Maliasili na utalii ikitamka kuwa baada ya kusitishwa kwa Operesheni Tokomeza, Tembo wawili huuawa na majangili kila siku. Hii haiukubaliki, kilichokosewa na kirekebishwe haraka na ianze tena kama alivyoahidi JK. 
Kwa upande wa barabara sioni kama kuna sababu ya Waziri Magufuli awajibike, kwa maana yeye amekuwa mstari wa mbele kusimamia sheria kibao kamataarifa hii niliyosoma mahali kuwa Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, amesema ataendelea kusimamia sheria ya barabara namba 30 ya mwaka 1973 hadi anaingia kaburini kwa kuhakikisha hakuna magari ambayo yanazidisha uzito na kuharibu barabara.
 “Nchini Ujerumani, uzito wa magari yote ni tani 40, Uingereza tani 40, Ufaransa 40, Urusi 38 lakini Tanzania tani 56, wakati mwingine tunakamata hadi tani 96,” aliongezea kwa kuwaga data kama kawaida yake katika taarifa hiyo. 

Hata hivyo nimesoma mahali pengine tena kuwa miezi miwili iliyopita Waziri Mkuu alisema sheria hiyo ilegezwe ili tume iundwe. Yaani magari yenye uzito yaendelee kutanua tukisubiri tume! 
JAMANI! HIVI KWELI TUSUBIRI TUME IUNDWE WAKATI BARABARA ZINAKUFA HIVI HIVI TUNAANGALIA KWA MANUFAA YA WACHACHE??? LET’S BE SERIOUS FOR ONCE! 
Hilo kaka halikubaliki. Nashauri wakati tume hiyo ikisubiriwa kuundwa (hata sijui ya kazi gani katika kuzuia uharibifu wa barabara, maana data hapo juu zinatusha) Dokta Magufuli aruhusiwe aendeleze juhudi zake za kukomboa barabara zetu. 
 Nasema hivi kwa sababu kama ilivyo katika kusitishwa Operesheni Tokomeza, barabara zetu zinaangamia kwa kilomita kibao kila dakika. Nimesoma mahali pengine kuwa gharama za kukarabati hizo barabara zilizoathirika kwa uzito wa magari ni takriban dola bilioni 350 ambazo ni hela za walipa kodi. Hili halikubaliki asilani!!! 
Namalizia kwa kumuomba Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Peter Kayanza Pinda afikirie upya swala la kulegeza sheria. Hapana. Asifikirie bali achukue hatua za haraka sana chini ya kauli mbiu ya BIG RESULTS NOW! 
Mdau Nehemia
Sao Paulo, Brazil
 Taswira hizi ni za barabara ya Morogoro road ambako sehemu kibao zimeharibika bila shaka kutokana na  uzito wa magari. Mwenye data atusaidie....





Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger