Na Athumani Shariff
Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe amekutana na balozi wa Ubelgiji Koen
Adam makao makuu ya Wizara ya Maji, Ubungo jijini Dar es Salaam kujadili mambo
mbalimbali yanayohusu sekta ya maji.
Profesa Maghembe alimuomba Balozi Adam asaidie wilaya ambazo zinakabiliwa na
matatizo makubwa ya uhaba wa maji, ambazo aliziainisha kuwa ni Makambako, Songea,
Wanging’ombe na Makonde ambapo jumla ya Dola 20,000,000 za Marekani zinahitajika
kutatua shida hizo.
Wakati wa mazungumzo hayo, Profesa Maghembe alisema wananchi haswa waishio vijijini
wanapata tabu sana kutokana na shida ya maji. “Wananchi wanapata tabu sana kupata
maji, inawagharimu kati ya saa moja hadi mbili kuchota ndoo moja ya lita ishirini, hivyo
ili kukamilisha mahitaji ya matumizi ni wazi kuwa muda mwingi utatumika na hatimaye
kuzorotesha shughuli nyingine za uzalishaji”. Alisema Waziri Maghembe.
Akijibu swali la Balozi Adam juu ya maswala ya umeme, Profesa Maghemebe alisema hiyo
ni changamoto kubwa sana kote mijini na vijijini. Gharama za Tanesco na zile za Diseli
zipo juu. Alisema tayari amemuagiza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mbogo
Futakamaba na baadhi ya wataalamu kutoka wizarani kwenda nchi za Uchina na Jamhuri ya
Watu wa Czech kutafuta kampuni zinazojishughulisha na umeme wa nguvu ya jua (Solar
Power) ili miradi yote ya maji vijijini itumie umeme wa jua ili kuwapunguzia gharama za
maji wananchi na hiyo kuifanya kuwa ndiyo sheria.
Waziri pia alieleza umuhimu wa upatikanaji wa maji safi katika kukabiliana na afya bora
kwa wananchi. Alisema, baada ya kuanza kutumika mradi mkubwa wa maji wa Kahama
Shinyanga sasa zaidi ya asilimia 80 ya watu hawendi hospitali juu ya magonjwa mbalimbali
yaliyokuwa yanawasumbua awali. Hivyo maji yanamchango mkubwa katika kuboresha afya
za wananchi alisisita Profesa Maghembe.
Pia alisema kwa kuwapatia wananchi huduma ya maji safi karibu na makazi yao ni njia
kubwa kutika kuwainua kiuchumi, kwani muda mwingi ambao wangeutumia katika kutafuta
maji watafanya shughuli nyingine za kiuchumi, hivyo kupandisha kipato chao.
Akielezea maswala ya utunzaji wa vyanzo vya maji, Profesa Maghemebe alisema ni moja ya
changamoto tunazokabiliananazo, maji hupungua ingawa mahitaji yawatu huongezeka hivyo
jitihada zetu kubwa sasa kwakupitia Idara ya Rasilimali za maji ni kutunza vyanzo vya maji
ili haya yaliopo sasa yaendeleee kuwepo kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo.
Post a Comment