Baadhi ya wanafunzi wa halaiki wa skuli mbali mbali za Zanzibar na Tanzania Bara wakijiandaa kwa ajili ya sherehe za mapinduzi ifikapo Januari 12 mwaka huu wa 2014.
Gari za Polisi zinazotumika wakati wa fujo na vurugu katika maeneo mbali mbali nchini zikiwa katika matayarisho ya mwisho kwa ajili ya sherehe za kutimia miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar zitakazofanyika huko uwanja wa Amani Mjini Zanzibar.
vijeba wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania {JWTZ } wakionyesha umwamba wao wakati wa matayarisho ya mwisho ya maadhimisho ya kutimia miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kifaru cha kivita cha JWTZ kikifanya matayarisho ya mwisho kwa ajili ya maadhimisho ya kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar zinazotarajiwa kufanyika uwanjani hapo Jumapili ya Januari 12 mwaka 2014.
Askari wastaafu wa Jeshi la Ukombozi la Unguja { JLU } ambalo linatarajiwa kuonyesha vitu vyao wakati wa kilele cha maadhimisho ya sherehe za kutimia miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makomandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania { jwtz } wakionyesha ustadi wao wakati wa mazoezi ya mwisho kwa ajili ya sherehe za kutimia nusu karne ya mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Post a Comment