Home » » Taarifa kuhusu Tsunami

Taarifa kuhusu Tsunami

Written By JAK on Wednesday, January 15, 2014 | 7:52 AM


TAARIFA
 
Kuna taarifa inayosambazwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu za mkononi (SMS) kuhusiana na TMA kutoa tahadhari ya Tsunami. Taarifa hizo sio za kweli, uonapo ujumbe huo, upuuzie kwa kuwa sio taarifa sahihi, 
ni taarifa ya upotoshwaji.
Taarifa rasmi ni kama ilivyotumwa awali kuhusiana na upepo mkali kwa Ukanda wa Bahari ya Hindi na Mvua kubwa kama inavyoonesha hapa:


Ujumbe huo unasomeka kama hivi:
TAHADHARI ya Tsunami: Kuanzia saa moja usiku
Tsunami itafika Tanzania na mawimbi yatakuwa makubwa
kuanzia muda huo. Taarifa zaidi itatolewa na Mamlaka ya
Hali ya Hewa Tanzania wakati wowote kuanzia sasa, kwa
mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agness Kijazi.
Tunapenda kuwataarifu wadau wetu kuwa ili kutoa taarifa sahihi ni 
vizuri kuwasiliana na Ofisi zetu kwa maelezo ya kina zaidi
 kuepusha mkangamanyo kwa wananchi.
Asante tena kwa ushirikiano wako,
Nakutakia Sikukuu njema ya Maulid,

Monica Mutoni
Ofisi ya Uhusiano
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger