Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe (kulia) akitoka katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam leo, ambapo aliwasilisha ombi la pingamizi la yeye kutojadiliwa kwenye kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kinachotarajia kufanyika kesho, hadi rufaa yake ya kupinga kuenguliwa wadhifa huo kwenye Baraza Kuu la chama hicho. Kushoto ni Wakili wa Zitto, Albert Msando. Mahakama Kuu imekubaliana na Zitto Kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kinachotarajiwa kufanyika kesho kutomjadili kwa namna yoyote
Wanasheria wa Chadema, Tundu Lisu (kushoto) na Peter Kibatala waliofika kupinga hoja hiyo mahakamani.
Tundu Lisu na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wakijadiliana jambo wakati wakisubiri uamuzi wa mahakama
Zitto ana wakili wake Msando wakiwasiliana na marafiki zao walipokuwa wakisubili uamuzi wa mahakama, ambapo Zitto aliibuka dedea kwa pingamizi lake kukubaliwa hivyo kikao cha Kamati Kuu kinachofanyika kesho kukatazwa kumjadili kwa namna yoyote Zitto. Picha na Kamanda wa Matukio
Post a Comment