Home » » Airtel yazindua huduma mpya ya Airtel money

Airtel yazindua huduma mpya ya Airtel money

Written By JAK on Tuesday, February 18, 2014 | 11:22 PM

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imetangaza rasmi huduma ya kisasa ya kifedha kupitia huduma ya Airtel Money. Huduma hiyo mpya ya kibunifu itatoa uzoefu tofauti wa huduma za fedha kwa wateja wake.

Akiongea wakati wa uzinduzi , Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Bwana Sunil Colaso alisema "leo tunayofuraha kuzindua huduma yetu mpya ya Airtel Money ijulikanayo kama "Hatoki Mtu Hapa", kwa mara ya kwanza nchini Tanzania wateja wa Airtel watafurahia kufanya miamala bure bila kikoma kwa kununua kifurushi cha Bure Pack cha wiki au cha mwenzi." 

Vifurushi vya Bure Packs vitawapa wateja wa Airtel Money uhuru wa kuchagua kifurushi kinachokidhi mahitaji yao na kuwawezesha kufanya miamala bure bila kikomo kwa wiki au kwa mwenzi kulingana na matakwa yao. 

Tumezindua huduma hii ili kuwapatia wateja wetu ubora, urahisi na unafuu katika kufanya miamala ya pesa.Kwa wateja ambao hawatajiunga na virufushi vya Bure Pack bado wataweza kufanya miamala ya pesa kwa bei nafuu kuliko zote ambapo kwa sasa watatozwa asilimia 50% yaani nusu bei ukilinganisha na gharama zinazotozwa na mitandao mingine. 

 Tunauhakika wateja wetu watafaidika sio tu kwa ubora, urahisi na ufanisi wa huduma yetu ya Airtel Money bali kwa kupata huduma zenye viwango nafuu zaidi, Akiongea kuhusu jinsi ya kupata huduma hiyo Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bi Beatirce Singano Mallya alisema "kujiunga na "Hatoki Mtu Hapa" packs wateja watalipia 1500 mara moja tu na kuendelea kufanya miamala bure bila kimomo kwa wiki nzima, vilevile watakaojiunga kwa mwenzi watalipia shilingi 5000 na kuendelea kufaidi huduma bure kwa mwenzi mzima".

"kwa ubunifu huu mpya huduma ya Airtel money bado itawawezesha wateja kupata huduma nyingine za ziada. Sasa wateja wa Airtel Money wanaweza kununua vifurushi vya Airtel Yatosha kwa namba zao au kwa namba ya mtu mwingine mahali popote , wakati wowote kupitia huduma ya Airtel money," aliongeza. 

Huduma ya "Hatoki Mtu Hapa" ni kwa wateja wote wa Airtel nchini , na kwa wateja wapya watakachotakiwa kufanya ni kutembelea Ofisi za Airtel au mawakala wa Airtel Money zaidi ya 35,000 walioko nchi nzima na kununua simcard mpya kisha kujisajili wakiwa na kitambulisho rasmi na kufurahia huduma. 

 Huduma ya Airtel Money imesaidia kuondoa changamoto za huduma za kibenki vijijini na mijini ambapo imewawezesha wateja kutuma na kupokea pesa bure, kulipia Ankara mbalimbali kama ada za shule, Visa ya US, bili ya maji DAWASCO, Umeme LUKU pamoja na DSTV. Ili kujiunga na huduma ya Airtel Money, Mteja anatakiwa kupiga *150*60# na kupata Menu ya Airtel Money.
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Bw Sunil Colaso akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel money ijulikanayo kama Hatoki Mtu Hapa  ambapo wateja watapa vifurushi vya BURE Packs vya kutuma pesa bure kwa wiki au Mwezi. Halfa ya huduma hii ilifanyika katika Makao makuu ya Airtel Leo
Mkurugenz Mtendaji wa Airtel Bw Sunil Colaso akionyesha kwa waandishi habari kipeperushi cha huduma ya Hatoki mtu hapa wakati wa uzinduzi,ambapo wateja watapa vifurushi vya BURE Packs vya kutuma pesa bure kwa wiki au Mwezi. Halfa ya huduma hii ilifanyika katika Makao makuu ya Airtel Leo.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger