Balozi wa mpya wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Aziz Ponary Mlima leo asubuhi ametembelea Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na kukutana na viongozi wa Ofisi hiyo.
Pamoja na mambo mengine waliozungumza, viongozi hao waliongelea diplomasia ya uchumi, maendeleo ya uchumi wa Tanzania na Malaysia kwa ujumla.
Dkt. Mlima aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka jana kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kuala Lumpur, Malaysia, ambayo imekuwa ikiisadia Tanzania katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo, ikiwemo utaratibu mpya wa kusamimia miradi ya maendeleo.
Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt Aziz Ponary Mlima (Kushoto) akizungumza na viongozi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Pamoja na mambo mengine waliozungumza, viongozi hao waliongelea diplomasia ya uchumi, maendeleo ya uchumi wa Tanzania na Malaysia kwa ujumla.
Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt Aziz Ponary Mlima (Kushoto) akiagana na Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt Philip Mpango mara baada ya mazungumzo yake na uongozi wa Tume.
Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Prof Longinus Rutasitara (Kulia) akichangia jambo wakati Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt Aziz Ponary Mlima (hayupo pichani) alipotembelea Tume ya Mipango kuonana na uongozi.
Picha na
SAIDI A. MKABAKULI
Post a Comment