Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi wa Manipal Hospital Ltd,alipotembelea katika Hospitali hiyo akiwa na Ujumbe wake jana,akiwa katika ziara ya siku tisa Nchini India.[Picha na Ramadhan Othman,India.]
Mkurugenzi Mtendaji wa Manipal Hospital Ltd ya Chuo cha kufundishia Madakatari Bw.Rajan Padukone,akitoa maelezo wakati wa Mkutano kati ya Uongozi wa Hospitali na Ujumbe wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipofika kutembelea Hospitalini hapo akiwa katika ziara rasmi nchini India.
Baadhi ya Maafisa waliofuatana na Rais wa wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika ziara rasmi nchini India wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyotolewa katika Mkutano wa pamoja walipofika kutembelea Hospitaliya Manipal Ltd
Mawaziri wa Wizara za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Muungano wakifuatilia vyema maelezo yaliyotolewa katika Mkutano wa pamoja Uongozi wa Manipal Hospital Ltd hapo jana wakiwa katika ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapainduzi Dk.Ali Mohamed Shein,ambayo inaendelea kwa siku tisa Nchini India ambayo ina malengo ya kukuza uhusiano na mashirikiano.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Uongozi wa Manipal Hospital Ltd,katika mkutano wa pamoja wa ushirikiano katika kuongeza utoaji wa huduma za Afya,akiwa katika ziara inayoendelea katika miji tofauti nchini India,yenye malengo ya kukuza uhusiano katika nyanja mbali mbali zikiwemo Kilimo, Afya na Biashara,(kushoto) Mkurugenzi Mtendaji wa Manipal Hospital Ltd Bw.Rajan Padukone
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk,Saleh Mohamed Jidawi,akitiana saini ya makubaliano na Mkurugenzi Mtendaji wa Manipal Hospital Ltd, Rajen Padukone katika Mji wa Bungaluru nchini India, makubaliano hayo yatanufaisha Madaktari wa Zanzibar kuja kujifunza kazi katika Chuo cha Hospitali hiyo,saini hiyo imetiwa wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwa katika ziara Nchini India. Picha na Ramadhan Othman wa Ikulu, Zanzibar
Post a Comment