Akizungumza katika warsha iliyofanyika mjini Iringa yenye lengo la kuwajengea uelewa wa katiba pamoja na mchakato wa marekebisho ya katiba kwa wananchi waishio wilaya ya Iringa vijijini, alisema kuwa viongozi wa Magereza waingizwe katika kamati ya ulinzi na usalama wa Taifa ili kuweza kutoa taarifa kwa kamati juu ya yanayotokea gerezani na wanayokabiliana nayo katika magereza.
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu John Msika alisema kuwa jeshi la magereza halijatajwa kama ni sehemu ya muungano hivyo halimtambui katika kuidhinisha adhabu.
“Mkuu wa jeshi la magereza aidhinishe kama mmoja wa wanakamati na mjumbe katika kamati kuu ya ulinzi na usalama “alisema Msika
Naye mkurugenzi wa mafunzo na utafiti Erick Nyato alisema kuwa Muundo wa serikali tatu utahimiza na kujari maadili na miiko ya viongozi wa umma kupunguza mamlaka ya Rais katika uteuzi wa viongozi mbali mbali.
Suala la serikali tatu sio kuvunja amani hili ni suala la uongozi kama itashindikana ni kubadilisha uongozi kwa sababu ni maamuzi yetu wenyewe wananchi .
Post a Comment