Home » » KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI APOKEA MITAMBO YA KUZALISHA UMEME JIJINI DAR LEO

KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI APOKEA MITAMBO YA KUZALISHA UMEME JIJINI DAR LEO

Written By JAK on Tuesday, February 18, 2014 | 11:01 PM

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. Eliachim Maswi (Kushoto) akipata maelezo mafupi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Bw. Felchesmi Mramba wakati wa Halfa ya kupokea mitambo miwili ya kuzalisha umeme yenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 183 itakayokwenda kufungwa Kinyerezi ambapo mitambo hiyo itaanza kufanya kazi mwezi wa kumi mwaka huu.Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. Eliachim Maswi akishuka kutoka juu ya meli wakati wa Hafla ya kupokea mitambo miwili ya kuzalishia umeme thamani ya Dola za Kimarekani milioni 183 kutoka kwenye Kampuni ya General Electronics ya Marekani inayokwenda kufungwa Kinyerezi,hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo.
Moja ya mitambo ya kuzalishia umeme ikipakiwa katika gari tayari kwa safari ya kwenda Kinyerezi kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi unaotarajiwa kuanza mwezi wa Tatu na kukamilika mwezi wa kumi mwaka huu, hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo (jana) ambapo mitambo hiyo imepokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. Eliachim Maswi. (Picha zote na Benjamin Sawe wa Maelezo).
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger