Home » » MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA OFISI YA IECO UKANDA WA AFRIKA JIJINI DAR

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA OFISI YA IECO UKANDA WA AFRIKA JIJINI DAR

Written By JAK on Thursday, February 6, 2014 | 6:23 AM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akikata utepe kufungua rasmi ofisi ya IECO ukanda wa Afrika, yenye makao yake makuu Beijing China iliyofunguliwa jijini Dar es Salaam Tanzania, leo Feb 5, 2014 kwa ajili ya kuwakilisha nchi za Afrika na tayari imeanza mchakato katika kukabiliana na magugu maji katika Ziwa Viktoria sambamba na shughuli nyingine zinazolenga utunzaji mazingira na namna ya kukabiliana na majanga yanayotokana na athari za tabia nchi. Kulia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia Sola Pawa ndogo maalum kwa kuchajia simu na kusomea baada ya kufungua rasmi ofisi ya IECO ukanda wa Afrika, yenye makao yake makuu Beijing China iliyofunguliwa jijini Dar es Salaam Tanzania, leo Feb 5, 2014 kwa ajili ya kuwakilisha nchi za Afrika. Kushoto ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akikabidhiwa Nembo ya Taasisi hiyo iliyofunguliwa jijini Dar es Salaam, leo.
Makamu wa Rais Dkt Bilal akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi na viongozi wa ofisi hiyo baada ya kufunguliwa rasmi, eneo la Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akiagana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka, baara ya uzinduzi huo. Picha na OMR
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger