Home » » Makete girls yamkuna mkuu wa mkoa wa Njombe

Makete girls yamkuna mkuu wa mkoa wa Njombe

Written By JAK on Thursday, February 13, 2014 | 12:28 AM

 Mkuu wa mkoa wa Njombe kapteni Mstaafu Aseri Msangi(katikati) akikagua majengo ya shule mpya wa wasichana wilayani Makete, kushoto ni mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro na kulia ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete Daniel Okoka.
 Ukaguzi huo ukiendelea.
 Wananchi wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni Msangi(hayupo pichani) akizungumza nao
 Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro akizungumza kwenye mkutano shuleni hapo
 Mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni Mstaafu Aseri Msangi akizungumza na wananchi shuleni hapo.
========  ======  =======
Habari/picha na  Edwin Moshi, Makete.

Kufuatia kukamilika kwa kiasi kikubwa majengo ya shule mpya ya sekondari ya wasichana Makete iliyojengwa katika kijiji cha Utweve kata ya Ukwama wilayani Makete, mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni mstaafu Asseri Msangi ameagiza shule hiyo iandikishwe ili ianze kutumika.

Mkuu wa mkoa ametoa agizo hilo hii leo Februari 11, 2014 wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya elimu wilayani Makete, ambapo baada ya kufika shuleni hapo ameridhishwa na ujenzi wa shule hiyo na kuona haina sababu ya shule hiyo kuendelea kukaa bila kuandikishwa ili ianze kupokea wanafunzi.

Akizungumza na wananchi wa vijiji viwili vinavyojenga shule hiyo ambavyo ni Utweve na Masisiwe, mkuu huyo wa mkoa mbali ya kupokea na kutjibu kero za wananchi, amekasirishwa na tabia ya wazazi wa vijiji hivyo kuwaambia watoto wao wafeli kwa makusudi ili wasiendelee na masomo ya sekondari.

"Ndugu zangu dunia tuliyopo sasahivi, si ile tuliyoishi zamani, mtoto asiposoma ni matatizo kwake, na ninyi wazazi wenye tabia ya kuwaambia watoto wenu wafeli kwa makusudi mnatupelekea taifa letu kaburini na sisi hatutakubali, tunaomba muiache hiyo tabia, somesheni watoto wenu" alisema Msangi.

Katika hatua nyingine Kapteni Msangi amechangia kiasi cha shilingi milioni 1 kwa ajili ya shule hiyo maalum kwa ajili ya wasichana kama njia mojawapo ya kusaidia ujenzi wa shule hiyo ambayo inatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Shule hiyo pekee ya wasichana wilayani Makete inajengwa na serikali kwa kushirikiana na wazawa wa Makete wanaoishi nje ya wilaya hiyo, wananchi pamoja na wadau mbalimbali.

Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger