Shughuli za Msiba wa Mama Theonestina Rweyemamu zinaendelea vizuri. Leo kutakuwa na misa ya Kumwombea Marehemu saa nne asubuhi kule Mount Vernon, New York na Anwani ya Kanisa ni kama ifuatavyo: The Sacred Heart Church, 115 Sharpe Blvd, South Mount Vernon, NY 10550.
Jana heshima za mwisho zilitolewa ambapo Watanzania wengi walifika kuuaga mwili wa Marehemu pale Camelot Funeral Home, 174 Stevens Avenue, Mount Vernon, NY 10550.
Chini ni taswira za picha za jana ni kama ifuatavyo:
Sehemu ya Watanzania waliohuzuria kama inavyoonekana kwenye picha. Katika mstari wa kwanza ni watoto wa marehemu na kutoka kushoto ni Diana, Doris na Emmanuel.
Katibu wa Jumuiya ya Watanzania New York, Deogratius Mhella naye aliiwakilisha Jumuiya ya Watanzania. Hapa alipata nafasi ya kusema machache.
Mama Balozi Mwinyi aliyekaa katikati naye alifika kutoa heshima zake za mwisho kwa marehemu na kuifariji familia ya mama Theonestina Rweyemamu.
Mama Kiswaga aliyesoma shule moja na Marehemu Theonestina naye akizungumza.
Post a Comment