Balozi wa Norway Nchini,Bi Ingunn Klepsvik (Katikati) akikagua baadhi ya
mabwawa ya ufugaji samaki manispaa ya Lindi walipotembelea mradi wa
uvuvi katika Ziara ya Mameya wa miji ya Norway waliokubali kujenga
urafiki na manispaa za Lindi na Mtwara,Kushoto ni Abdilah Salum
mmiliki wa mabwawa hayo na Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi Dr Nasor
Hamid.
Balozi wa Norway Nchini,Bi Ingunn Klepsvik akipokea maelezo ya hali ya Uvuvi Ndani ya
manispaa ya Lindi toka mkurugenzi wa manispaa Kelvin Makonda huku
mmiliki wa mabwawa hayo akielezea mipango yake ya baadae ikiwa pamoja
na kuiomba Norway kumsaidia Elimu na utaalamu bora wa ufugaji wa
Kisasa.
Mabwawa yanayotumika kwa ufugaji wa samaki.
Meya wa manispaa ya Alstahaug,Bard Anders Lango
akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi,Dk. Nassor Hamid wakibadilishana mawazo juu ya
Ushirikiano huo ikiwemo Uwekezaji katika mji wa Lindi ambao hauna hata
kiwanda kimoja hadi sasa huku kukiwa na harakati za kujengwa kwa
kiwanda cha simenti cha Meis kitakachochangia ajira mbalimbali.
Meya wa manispaa ya Hammerfest Alf E Jakobsen
(kati)akisikiliza maelezo ya Ufugaji wa samaki toka kwa Afisa Uvuvi wa
manispaa ya Lindi Bi Sharifa Tomera.
Ujumbe toka Norway wakipata maelezo ya ukaushwaji wa
samaki kwa njia ya kienyeji kutokana na kukosa dhana bora.
Na ABDULAZIZ ,Lindi
Miji miwili ya Hammerfest na Sandnessjoen iliyoko nchini Norway
Imekubali kuanzisha ushirikiano baina ya manispaa ya Lindi na Mtwara
Ambapo kwa pamoja wameitaka Halmashauri ya Manispaa ya Lindi pamoja
na wanajamii kuwekeza katika Elimu ikiwemo kujijengea Tabia ya Kulipa
kodi ambazo zitarudi katika huduma za jamii.
Uamuzi huo umefikiwa katika mkutano baina ya viongozi wa miji hiyo na
Manispaa hiyo baada ya kutembelea miradi mbalimbali ya Gesi na Uvuvi
vitu ambavyo vinachangia pato kubwa katika Nchi zao.
Katika makubaliano hayo viongozi kutoka pande zote wamekubaliana kuwa
mji wa Harmmerfest utashirikiana na Lindi na ule wa Sandnessjoen
utashirikiana na Mtwara, ushirikiano ambao unalenga kuzitumia fursa
zilizopo kujikwamua kiuchumi kupitia sekta hizo ili kuhakikisha mikoa
ya kusini inanufaika na rasilimali zake ikiwemo Ardhi ya kutosha na
fukwe zenye ubora.
Akizungumzia umuhimu wa makampuni ya mafuta katita mji wa Sandnessjoen
Meya wa mji huo Bard Anders Lango ameeleza kuwa mji wake unanufaika na
mafuta na asilimia kubwa ya wananchi ni walipa kodi na asilimia 12 ya
mapato urudishwa katika huduma za jamii zikiwemo Elimu na Afya.
Akiongea na globu hii,Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Lindi Kelvin
Makonda kwa Upande wake ametoa Shukrani kwa ujio huo na Kuanzishwa kwa
ushirikiano baina ya miji hiyo na mikoa ya kusini kutasaidia kufungua
ukurasa mpya wa mahusiano na kuwezesha wananchi kuwa sehemu ya
mafanikio ya kuanzishwa kwa miradi ya umma katika maeneo yao.
Huu ujio umekuja muda muafaka huku manispaa yangu kwa kushirikiana UTT
tayari imepima Viwanja vya kutosha na tumeanza mchakato wa kuviuza na
hata hawa wageni wetu tumewapa Fursa ya kununua viwanja kwa ajili ya
shughuli za uwekezaji ikiwemo Hotel,Elimu na Viwanda maeneo yapo ya
kutosha".
Katika ziara hiyo inayoongozwa na Balozi wa Norway nchini Tanzania,Bi
Ingunn Klepsvik walitembelea Mabwawa ya Uvuvi ya ASM Trading 2005 na
kumilikiwa na Abdillah Salum Mfaume ambayo tayari jumla ya Samaki
96468 wameshapandwa katika mabwawa hayo.
Aidha Bw Abdilah salum alitoa wito kwa ugeni Huo kusaidiwa utaalam wa
kutosha katika Ufugaji wa Kutosha bila ya kuathiri Mazingira na
kubainisha kuwa matarajio yake ni kuvuma zaidi ya kilo 25000 katika
kipindi cha miezi sita ijayo hali itakayomwongezea kipato na
kujiwezesha kuboresha Uvuvi katika mkoa wa Lindi
Post a Comment