Mkuu
wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza akimuonesha Waziri wa Maji, Profesa Maghembe
samaki waliokufa katika bwawa linalosadikiwa kutiwa sumu na mtu asiyejulikana.
Mto Wame ambao ndiyo chanzo kikuu cha maji cha
mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Chalinze jinsi ulivyochafuka.
Mkurugenzi wa majisafi na usafi wa mazingira
Chalinze Christa Mchomba akimuonesha Waziri wa Maji Profesa Jumanne maghembe na
aliyoongozana nao jinsi mto Wame ulivyochafuka, aliyeinama ni Mkuu wa Mkoa wa
Pwani Mwantumu Mahiza.
Waziri
wa maji Profesa Jumanne Maghembe, akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kibindu wilayani
Bagamoyo. Waziri aliwahakikishia kisima cha maji katika kijiji chao.
* Atoa
maagizo kwa kwakurugenzi na wahandisi wa maji
*Ajionea
Maji yalivyochafuko mto Wame
Na
Athumani Shariff
Waziri
wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe, amefanya ziara Mkoani Pwani ili kukagua na
kutoa maelekezo katika miradi ya maji ya Mkoani humo.
Katika
ziara hiyo iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza, ilikagua
miradi mbalimbali ya maji katika maeneo ya Chalinze, Visiga, Vigwaza, Kibinda
na mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Chalinze.
Profesa
Maghembe pia alitembelea bwawa la maji la Pigo shule ilikagua na kujionea hali
ya bwawa hilo lililotiwa sumu na watu wasiojulikana.
Bwawa
la Pigo linasadiwa kuwa limetiwa sumu na watu wasiojulikana kutoka na maji yake
kuwa na mapovu huku samaki na vyura kufa na kuonekana wakielea katika bwawa
hilo.
Akiueleza
msafara huo, Waziri Maghembe alisema, tayari ameshawaagiza wataalamu wa maabara
ya maji kutoka Wizara ya Maji ili wakayakague maji hayo, lakini wananchi
wasiyatumie maji haya.
Profesa
Maghembe pia alimuagiza Mkurugenzi wa Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira
chalinze Christa Mchomba, ahakikishe watu waishio maeneo hayo hawapati mgao wa
maji ili wasiende kuchota maji hayo yenye sumu.
“Mkurugenzi
hakikisha wananchi hawa hawapati mgao wa maji ili wasijekuchota maji haya”
alisisitiza Waziri Maghembe.
Pamoja
na miradi hiyo, Waziri pia alitembelea na kujionea jinsi mto Wame
ulivyochafuka. Mto Wame ambao ndiyo chanzo kikuu cha maji cha Mamlaka ya
majisafi na usafi wa mazingira Chalinze umechafuka kutoka na shughuli za
kibinaadamu zinazofanywa kwenye vyanzo vyake vya Mkoani Morogoro.
Akieleza
katika ziara hiyo Mkurugenzi wa Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira
Chalinze, Christa Mchomba alisema “Mto Wame umechafuka sana hali ambayo haijawahi
kutokea tangu kuanza kwa mamlaka hii ya maji ya Chalinze. Maji yamekuwa tope
kutokana na shughuli za kibinaadamu zinazofanywa hasa katika vyanzo vya
Morogoro.
Kutokana
na uchafuzi huo uliopelekea maji kuwa tope uzalishaji wa maji umepungua hadi kufikia
asilimia 8 kitu ambacho kimepelekea mgao wa maji katika maeneo mengi yaliyokuwa
yakipata huduma ya maji kupitia mamlaka hiyo.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, alimshukuru Waziri wa Maji kwa kutenga muda wake
ili kutembelea miradi ya maji katika wilaya ya Bagamoyo.
“Kwa
niaba ya wananchi wa Bagamoyo, nakushukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa
kwakutenga muda wako kuja kututembelea na kujionea miradi ya maji katika
Halmashauri yetu.
Post a Comment