Pages

Monday, February 10, 2014

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MH. MATHIAS CHIKAWE AKUTANA NA MWAKILISHI MKAZI WA UNHCR TANZANIA

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi aliyekaa kutoka kushoto  Mh, Mathias Chikawe akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu shughuli za Idara ya Wakimbizi kwa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR nchini Tanzania  Joyce Mends-Cole aliyekaa kati kati. Mwakilishi huyo alimtembelea Waziri Chikawe leo katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ili kujitambulisha kwa Waziri huyo ambaye ameteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Jakaya Kikwete  kuiongoza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.   
Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mathias Chikawe akimsikiliza kwa Makini Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi nchini Tanzania UNHCR Joyce Mends-Cole aliyekaa kati kati  wakati mwakilishi huyo alipomtembelea leo Waziri Chikawe kwa ajili ya kujitambulisha ikiwa ni Siku chache baada ya Waziri Chikawe kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuiongoza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment