Home » » MWANAMAMA MJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA AJITOSA KUWANIA UMAKAMU MWENYEKITI

MWANAMAMA MJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA AJITOSA KUWANIA UMAKAMU MWENYEKITI

Written By JAK on Thursday, March 13, 2014 | 8:33 PM

 
 Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Thomas Kashilila akitoa maelekezo kwa wapambe wa mgombea Nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba kabla ya kupokea Fomu hizo Mapema Leo asubuhi Mjini Dodoma

Kina Mama wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakimsindikiza Mjumbe wa Bunge Hilo na Mgombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Bi. Samia Suluhu Hassan(Aliyenyanyua fomu)kurudisha fomu kwa Katibu wa Bunge Mapema Leo asubuhi Mjini Dodoma.

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Bi. Samia Suluhu akizipitia Fomu kabla ya Kuzikabidhi kwa Katibu wa Bunge tayari kwa uchaguzi utakaofanyika joini ya leo Mjini Dodoma.

Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Thomas Kashilila akisaini fomu za mgombea Nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mapema Leo asubuhi Mjini Dodoma.

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Bi. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi fomu Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Thomas Kashilila (Kulia) Mapema Leo asubuhi Mjini Dodoma.

Kina Mama wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakiimba kwa furaha baada ya fomu za Mgombea wa Nafasi ya Makamu Mwenyekiti Samia Suluhu Hassan Mapema Leo asubuhi Mjini Dodoma.(PICHA NA HASSAN)
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger