Home » » SAMUEL SITTA AWA MWENYEKITI WA KUDUMU WA BUNGE MAALUM LA KATIBA

SAMUEL SITTA AWA MWENYEKITI WA KUDUMU WA BUNGE MAALUM LA KATIBA

Written By JAK on Wednesday, March 12, 2014 | 9:14 PM

Mgombea wa nafasi ya Uenyekiti wa Kudumu wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta ameshinda nafasi hiyo kwa kura 487 dhidi ya mpinzani wake, Mhe. Hashim Rungwe aliyepaya kura 69 kati ya kura 593 zilizopigwa, na saba kuharibika katika uchaguzi uliofanyika muda mfupi uliopita Bungeni mjini Dodoma.

Akitoa Neno la Shukrani mara baada ya kupata nafasi hiyo,Mh. Sitta amewashurukuru Wajumbe wote wa Bunge la Katiba kwa kuweza kumpa nafasi hiyo adhimu. Pia amempongeza mpinzani wake,Mh. Hashim Rungwe kwa kukubali matokeo hayo.



 Wajumbe wakipiga kura

 Upigaji kura ukiendelea



Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakimpongeza Mhe. Sitta kwa ushindi wake wa kishindo

Mikono ya pongezi yazidi kumiminika

Mwenyekiti wa Kudumu wa Bunge Maalum la Katiba mteule Mhe Samwel John Sitta akitoa neno la shukurani kwa Wajumbe kwa imani waliyoonesha kwake kwa kumchagua kwa kura nyingi kushika nafasi hiyo. Picha zote na Deusdedit Moshi wa Globu ya Jamii, Dodoma
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger