Home » » KONGAMANO LA MAFUTA NA GESI BERLIN UJERUMANI LAZINDULIWA NA PROFESA MUHONGO

KONGAMANO LA MAFUTA NA GESI BERLIN UJERUMANI LAZINDULIWA NA PROFESA MUHONGO

Written By JAK on Saturday, April 26, 2014 | 1:15 AM


 
Waziri  wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akifungua kongamano hilo ikiwa ni pamoja na kuwasilisha mada juu ya fursa za uwekezaji nchini Tanzania katika sekta za mafuta, gesi ikiwa ni pamoja na madini.

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Philip Marmo akifungua kongamano hilo

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (Mb.) (kushoto) akisalimiana na mmoja wa wajumbe anayewakilisha wafanyabiashara kabla ya kufungua kongamano la  mafuta na gesi linaloendelea huko Ujerumani  kama moja ya   maadhimisho ya muungano wa Tanganyika na  Zanzibar

Mtaalamu kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini  (TPDC) Bi Venosa Ngowi (kulia) akimweleza Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (mwenye suti nyeusi) shughuli zinazofanywa na shirika hilo kwenye maonesho yanayoendelea huko Berlin, Ujerumani.  Pembeni ya Waziri ni Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Philip Marmo.

Mtaalamu kutoka Wakala wa Jiolojia Nchini (GST) Bi. Augustina Rutaihwa akitoa maelezo kwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) juu ya shughuli zinazofanywa na wakala huo. Kushoto mwa Waziri ni Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Philip Marmo.

Kikundi cha  ngoma za sanaa kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania kikitumbuiza kabla ya kuanza kwa kongamano hilo
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger