Home » » MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA HOSPITALI YA MKOA WA LINDI NA KUPOKEA MBIO ZA PIKIPIKI KUADHIMISHA MIAKA 50 YA MUNGANO

MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA HOSPITALI YA MKOA WA LINDI NA KUPOKEA MBIO ZA PIKIPIKI KUADHIMISHA MIAKA 50 YA MUNGANO

Written By JAK on Friday, April 18, 2014 | 9:04 PM



Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete akimjulia hali mtoto Seleman Salum Namputa, miezi 3, aliyelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Lindi, Sokoine. Kulia ni Mama mzazi wa mtoto Seleman ajulikanaye kama Mariam kutoka katika kijiji cha Moka huko Lindi Vijijini. Mama Salma alitembelea hopitalini hapo tarehe 18.4.2014.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)  wa Lindi Mjini na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimsikiliza kwa makini mtoto Idd Omar kutoka katika Kijiji cha Madangwa , kata ya Sudi huko Lindi Vijijini. Mama Salma alifika kijijini hapo kwa ajili ya kupokea mbio za uzalendo za pikipiki zilizoandaliwa na Umoja wa Vijana, (UVCCM) kitaifa zikitokea Mkoa wa Mtwara tarehe 17.4.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwaelekeza baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Madangwa namna ya kushika mfagio ili usiweze kuleta madhara kwa watoto waliobeba na hata wengine na pia ni njia bora ya kulinda afya zao kwani wakishika upande unaotumika kufagia wanaweza kupata magonjwa ya kuambukizwa. 

Baadhi ya wasichana na akina mama wakionyesha umahiri wao katika kucheza ngoma za utamaduni wakati wa sherehe ya makabidhiano ya mbio za pikipiki kutoka mkoani Mtwara kwenda Mkoa wa Lindi katika Kijiji cha Madangwa tarehe 17.4.2014.

Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mtwara Ndugu Mohamed Said Sinani (mwenye kofia) akifuatana na viongozi wenzake wa Chama Cha Mapinduzi na Umoja wa Vijana kwenda kukabidhi mbio za pikipiki kwa uongozi wa Mkoa wa Lindi kwenye Kijiji cha Madangwa tarehe 17.4.2014.
 

Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Mtwara ndugu Mohamed Sinani  akikabidhi picha ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi Mzee Ali Mtopa na picha ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mheshimiwa Abeid Aman Karume kwa Mama Salma Kikwete kuashiria muendelezo wa mbio za uzalendo za pikipiki kusherehekea miaka 50 ya Mungano wa Tanganyika na Zanzibar hapo tarehe 26.4.2014.
 
Mjumbe wa NEC wa Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Madangwa na wageni waliohudhuria sherehe ya kupokea mbio za pikipiki kwa Mikoa ya Kanda ya Kusini inayojumuisha Ruvuma, Mtwara na Lindi katika kusherehekea miaka 50 ya Mungano.



Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM, Mama Salma Kikwete akiwahutubia wananchi wa Kata ya Mingoyo wakati wa sherehe ya mbio za pikipiki kusherehekea miaka 50 ya Mungano zitakazofikia kilele tarehe 26.4.2014.

Viongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi kutoka Mikoa ya Lindi na Mtwara wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiana mbio za pikipiki kusherehekea miaka 50 ya Mungano.
 
Bwana Salum Musa Mtungulu mkazi wa Kijiji cha Madangwa alitumia fursa hiyo ya makabidhiano ya mbio za pikipiki kurejea Chama Cha Mapinduzi akitokea Chama Cha NCCR- Mageuzi. Katika picha hiyo anatoa maelezo  ya kitendo hicho huku makada wakimvisha mavazi ya Chama Cha Mapinduzi.

Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM kutoka Lindi Mjini, Mama Salma Kikwete akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Mnazi Mmoja  kilichoko katika Kata ya Mingoyo walifurika kushuhudia sherehe za mbio za pikipiki za uzalendo kusherehekea miaka 50 ya Mungano .

Baadhi ya wasichana na akina mama wakionyesha umahiri wao katika kucheza ngoma za utamaduni wakati wa sherehe ya makabidhiano ya mbio za pikipiki kutoka mkoani Mtwara kwenda Mkoa wa Lindi katika Kijiji cha Madangwa tarehe 17.4.2014.


 PICHA NA JOHN LUKUWI. 
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger